Serikali ya Eritrea imepiga marufuku ndege za Ethiopia, Ethiopian Airlines kuingia nchini mwake ikilaumu huduma mbovu.
"Kwa kutambua desturi potofu zinazofuatiliwa na Shirika la Ndege la Ethiopia kwa ujumla na kwa utaratibu na kwa mpangilio wa ripoti za mizigo na hasara ya muda mrefu, bila kulipwa fidia hasa ikiambatana na kupanda kwa bei na makosa mengine yasiyo ya msingi," imesema taarifa kutoka Mamlaka ya Angani ya Eritrea.
Mamlaka hiyo imesema kumekuwa na maombi ya mara kwa mara kwa kampuni ya ndege ya Ethiopia kurekebisha malalamiko hayo na changamoto nyengine lakini haijapata majibu yanayofaa.
"Kwa kuzingatia hili, Mamlaka ya Anga ya Eritrea inalazimishwa kusimamisha safari zote kupitia ndege ya Ethiopian kwenda Eritrea kuanzia 30 Septemba 2024," taarifa imeongezea.
Imeomba wasafiri wote wanaoelekea Eritrea kufanya mabadiliko yanayofaa kwa usafiri wao na kutafuta namna nyengine.
Kampuni ya ndege ya Ethiipai imesema imepokea taarifa hiyo lakini haielewi sababu.
" Sababu mahususi za kusimamishwa huku hazijafichuliwa kwetu. Shirika la Ndege la Ethiopia kwa sasa linatafuta ufafanuzi kutoka kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Eritrea na imejitolea kutatua masuala yoyote kwa amani na haraka," imesema katika taarifa.
Hii ni mara ya pili ya uhasama wa angani kati ya nchi hizo mbili.
Kampuni ya Ndege ya Ethiopia ilifanya safari yake ya kwanza kwenda Eritrea 18 Julai 2018. Hii ilikuwa miaka 20 tangu nchi hizo kusitisha usafiri huo kwa sababu wa uhasama wa kisiasa.
Hii iliangaliwa kama mchango mkubwa wa kuvunja uadui kati ya nchi hizo mbili ambazo zilikuwa moja kabla ya 1991.
Julai 2, mwaka huo wa 2018, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliwasili katika mji mkuu wa Eritrea Asmara kutia saini makubaliano ya kihistoria na Rais Isaias Afwerki, kumaliza rasmi "hali ya vita" kati ya mataifa yao.