Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini Kenya, KWS, lilimuokoa duma mwenye umri wa miezi minne ambaye alipatikana akiwa ametelekezwa na mama yake katika wadi ya Sankuri kaunti ya Garissa.
"Mtoto huyo kwa sasa anatunzwa na timu katika kituo cha Garissa KWS kwa uhusiano na wataalamu wetu wa mifugo ambao wanampa mtoto huyo uangalifu wa kila saa," KWS imeelezea katika taarifa.
Duma huyo pia anapewa pia maziwa ambayo ni lishe bora.
"Mtoto huyo atahamishiwa katika Kituo cha Mayatima cha Wanyama cha Nairobi kwa malezi," KWS imeongezea.
KWS ina sema iko katika harakati za kukamilisha mpango kazi wa kitaifa wa uhifadhi wa duma.
TRT Afrika