DRC: Mashirika ya kibinadamu wanahitaji dola milioni 361 ili kukabiliana na majanga ya Ituri.

DRC: Mashirika ya kibinadamu wanahitaji dola milioni 361 ili kukabiliana na majanga ya Ituri.

Watu takriban milioni 4.5 wamekimbia makazi yao kutokana na mapambano yanayoendelea nchini
Wakimbizi kambi ya Rhoe, mkoa wa Ituri | Picha: OCHA

Katika taarifa ya OCHA ambayo TRT Afrika ilipokea nakala yake, ilisema mashirika yaa kibinadamu wanahitaji milioni 361 za dola ili kusaidiya watu milioni 1.1 walio hatarini katika jimbo la Ituri mashariki mwa Congo.

Tangazo hili linakuja siku chache baada ya mashambulizi ya waasi katika maeneo kadhaa ya Ituri ilio sababisha kupoteza kwa maisha ya watu takriban 150 katika wiki mbili za kwanza za Aprili.

"Waasi walishambulia miji ya Djugu, Irumu na Mambasa katika kipindi cha kuanzia Aprili 1 hadi 14. Mashambulizi haya yalisababisha kuhama kwa zaidi ya raia milioni 1.6 kuelekea mji wa Bunia. Vituo kadhaa vya afya vilibomolewa wakati wa mashambulizi haya," taarifa imeongezwa.

Kama ukumbusho, eneo la mashariki mwa DRC inatikiswa na mashambulizi ya makundi ya waasi, ambayo, kulingana na Kamishna Mkuu wa Wakimbizi, karibu watu milioni 4.5 tayari wamekimbia makazi yao kwa sababu ya vita.

TRT Afrika