Mwaka 2024 mipango ya msaada kwa ajili ya waliaothirika nchini Ethiopia inakadiriwa kuwa dola bilioni 3.24 kwa mwaka 2024 lakini chini ya asilimia 5 imefadhiliwa.
Serikali ya Ethiopia na washirika wa kimataifa wanakutana leo mjini Geneva, nchini Switzerland ili kuongeza uungwaji mkono wa kimataifa huku mpango wa kukabiliana na misaada ya kibinadamu.
Serikali za Ethiopia na Uingereza pamoja na Umoja wa Mataifa zinapanga mkutano huo ambapo matangazo ya ufadhili unatarajiwa kutoka nchi tofauti.
Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu wanaunga mkono juhudu za kimataifa kwa ajili ya kutoa msaada wa kuokoa maisha ya watu milioni 15.5, na msaada wa chakula wa dharura kwa hadi watu milioni 10.4.
Ili kutoa msaada wa haraka na kuhakikisha msaada endelevu kwa miezi mitano ijayo, dola bilioni 1 zinahitajika.
Hali ngumu ya maisha imeathiriwa kwa sababu tofauti zikiwemo ukame na mafuriko, na migogoro.
Shirika la UN la kibinadamu, UNOCHA, inasema ukosefu wa usalama wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kilele kwa watu milioni 10.8 wakati wa msimu wa Julai hadi Septemba.
Inaongeza kuwa baadhi ya watu milioni 4.5 wamekimbia makazi yao na kuna wasiwasi unaoongezeka kuwa afya ya watu na ulinzi kuzorota.
"Hali ya El Niño imezidisha ukame katika nyanda za juu kaskazini na mamilioni ya watu wanakabiliana na maji kidogo, malisho makavu na mavuno madogo. Viwango vya utapiamlo katika sehemu za Afar, Ahmara, Tigray na mikoa mingine vinatia wasiwasi mkubwa na vinaendelea kuwa mbaya zaidi," UNOCHA inasema katika taarifa.
Wakati huo huo, miaka miwili ya vita kasakazini mwa nchi hiyo katika eneo la Tigray na mikoa mingine imeharibu maelfu ya shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya jamii.
Hivi majuzi Serikali ya Ethiopia iliidhinisha Sera na Mkakati mpya wa Kitaifa wa Kudhibiti Hatari za Maafa kwa kutambua uwezekano wa nchi hiyo kukabiliwa na majanga mbalimbali ya hali ya hewa na migogoro.
Ethiopia pia imetoa dola milioni 250 kwa ajili ya msaada wa chakula katika miezi ijayo na rasilimali zaidi za ndani zimetolewa kwa ajili ya kukabiliana na dharura kutoka kwa serikali za kikanda na sekta binafsi ya Ethiopia.
"Ethiopia imeazimia kumaliza mzunguko wa uhaba wa chakula. Tunashukuru kuendelea kuungwa mkono na washirika wetu wa maendeleo ," balozi Taye Atske Selassie waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia amesema.