Na
Mazhun Idris
Ni kawaida kabisa kukutana na mgahawa unaouza Attieke katika kila kona za mtaa wa Anyama-Adjamé, jijini Abidjan, nchini Ivory Coast.
Hata kwenye kaya mbalimbali, Attieke ni kitu kawaida kukiona mezani.
Ukijulikana pia kama "garba", chakula hicho cha kitamaduni kimekuwa ni sehemu ya utamaduni wa Ivory Coast, kwa karne na karne.
Mara nyingi, Attieke huchanganywa na samaki aliyekaangwa au nyama, pamoja na mchuzi na mboga zingine.
Umaarufu kimataifa
Disemba 5, 2024, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), lilikiorodhesha chakula cha Attieke kama sehemu ya urithi wa kiutamaduni. Hadhi hiyo, inaufanya mlo huo kuwa kati ya vyakula vinavyopendwa zaidi barani Afrika.
UNESCO pia imetambua namna ya kutayarisha chakula hicho, hasa na wanawake na wasichana wa Afrika Magharibi.
UNESCO imekipa chakula hicho kinachotengenezwa na mihogo.
Mbali na kuwa alama ya utamaduni, chakula hiki pia huchangia kipato cha wanawake na wasichana nchini Ivory Coast.
Uamuzi wa UNESCO unaamanisha ni vyema asili ya mlo huo ukahifadhiwa kwa ajili ya vizazi na vizazi.
Mapema mwaka 2024, shirika la hakimiliki lilisajili alama ya biashara yenye kuzuia vyakula vingine vitokanavyo na mihogo kuitwa Attieke.
Mseto wa vyakula vya Kiafrika
Orodha hiyo ya UNESCO huishwa kila mwaka, ikihusisha vyakula, vinywaji na stadi mbalimbali.
Afrika inasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya vyakula mbalimbali vinavyozalishwa kutoka Johannesburg hadi Cairo, Mogadishu mpaka Nouakchott.
Vyakula vingine vilivyomo kwenye orodha ya UNESCO ni pamoja na Harissa, chakula kutoka Tunisia kinachosifika kwa kuwa na pilipili nyingi na Nsima unga wa ugali kutoka Malawi.