Maeneo manne ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda yametambuliwa katika Urithi wa Dunia na UNESCO.
Kati ya Aprili na Julai 1994, takriban watu milioni moja waliuawa nchini Rwanda na watu wenye silaha walioitwa Interahamwe, watu hawa waliwalenga wale wa kabila la Watutsi, lakini pia waliwaua wa kabila la Wahutu na Watwa ambao walikuwa na msimamo wa wastani.
Waathiriwa wa mauaji ya kimbari wanakumbukwa katika maeneo haya manne ya kumbukumbu.
"Kutambuliwa huku kunatupa motisha ya mapambano ya kukana Mauaji ya Kimbari na kutusaidia kuelimisha vizazi vya sasa na vijavyo," Waziri wa Umoja wa Kitaifa na Ushirikiano wa Kiraia Jean Damascene Bizimana alisema.
Maeneo haya manne ni yapi?
Katika kilima cha Gisozi katika katika mji mkuu wa Rwanda , Kigali, katika kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali iliyojengwa mnamo 1999, zaidi ya watu 250,000 wamezikwa katika eneo hilo.
Zaidi ya watu 50,000 wa mauaji ya Kimbari wamezikwa katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Murambi yaliyotokea katika wilaya ya Nyamagabe.
Ilikuwa Shule ya Ufundi, ambayo iligeuzwa kuwa mahali pa mauaji mwaka 1994.
Takriban miili 1,200 ilihifadhiwa pamoja na mali zao ikiwemo nguo kama ushahidi wa mauaji ya halaiki yaliyotokea katika eneo hilo.
Kanisa katoliki lililojengwa katika kilima cha Nyamata mwaka1980 ni mojawapo ya maeneo yaliyofanyika mauaji.
Mnamo 1994, zaidi ya watu 40,000 waliokuwa wametafuta hifadhi huko wote waliuawa kikatili kwa siku moja.
Katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Bisesero Rwanda inaikumbuka kama "Kumbukumbu ya Ushujaa".
Hapa watu wa kabila la Watutsi walipigana na washambuliaji wa Interahamwe kwa siku nyingi hadi hapo wauaji walipopata msaada kutoka kwa wanajeshi wa Ufaransa.
Katika eneo hili kati ya miezi ya Mei na Juni 1994, Interahamwe iliua zaidi ya Watutsi 40,000.
,