Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi (CENI) imetangaza ratiba ya uchaguzi wa wabunge, wilaya na vijiji nchini humo, shirika la habari la Xinhua limeripoti.
Tangazo hilo lilitolewa wakati wa mkutano wa pamoja kati ya tume hiyo na wadau muhimu wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa, maofisa wa serikali na wanadiplomasia wanaofanya kazi zao nchini Burundi.
“Katika wasilisho letu, tumewaonesha washiriki vituo vya kuandikishia wapiga kura ambavyo baadaye vitakuwa vituo kamili vya kupigia kura. Pia tumewapa ratiba nzima,” Mwenyekiti wa CENI Peosper Ntahorwamiye aliwaambia waandishi wa habari.
Kulingana na Ntahorwamiye, uchaguzi wa wabunge na madiwani wa wilaya utafanyika kwa pamoja Juni 5, 2025.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa CENI, uchaguzi wa maseneta utafanyika Julai 23, 2025 wakati ule wa wawakilishi wa vijiji, unapangwa kunayika Agosti 25, 2025.