Rais wa Marekani Joe Biden aliteua Kenya kama "mshirika mkuu asiye wa NATO" siku ya Jumatatu, na kuifanya kuwa taifa la kwanza la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupokea hadhi hio.
"Kwa mamlaka niliyopewa kama Rais na Katiba na sheria za Marekani, ikiwa ni pamoja na kifungu cha 517 cha Sheria ya Usaidizi wa Kigeni ya 1961, kama ilivyorekebishwa (22 U.S.C. 2321k), ninateua.Kenya kama Mshirika Mkuu Asiye wa NATO wa Marekani kwa madhumuni ya Sheria ya Kudhibiti Usafirishaji wa Silaha," ilisema risala ya White House.
Biden alitangaza kwa mara ya kwanza uamuzi wa kuiteua Kenya, mwezi wa Mei alipokuwa mwenyeji wa Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya White House kwa ziara ya kifahari huku wakisherehekea miongo sita ya uhusiano.
Hatua hiyo inakuja wakati Marekani inataka kupigana dhidi ya ushawishi wa Urusi na China katika eneo hilo.
Biden kisha akaashiria usaidizi wa Nairobi kushirikiana katika kuipa vipaumbele usalama wa taifa la Marekani, ikiwa ni pamoja na juhudi za kulishinda kundi la kigaidi la Daesh/ISIS pamoja na al-Shabab katika Afrika Mashariki, na kile Biden alichoeleza kuwa "kusaidiana" katika suala la Ukraine na juhudi zinazoendelea za kupeleka kikosi cha usalama cha Kenya katika taifa la Haiti lililokumbwa na machafuko.
Washirika wengine wakuu wasio wa NATO ni pamoja na Argentina, Australia, Bahrain, Brazil, Colombia, Misri, Israel, Japan, Jordan, Kuwait, Morocco, New Zealand, Pakistan, Ufilipino, Qatar, Korea Kusini, Thailand na Tunisia. Taiwan inachukuliwa hivyo bila kuteuliwa rasmi.