Bernard Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje Tanzania Afariki Dunia

Bernard Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje Tanzania Afariki Dunia

Membe alihudumu kama waziri wa mambo ya nje nchini Tanzania katika kipindi cha mwaka 2007 hadi 2015
Waziri wa zamani wa Tanzania afariki dunia Picha Bernad Membe Twitter

Bernad Membe ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 69.

Kwamujibu wa taarifa zilizo ripotiwa na vyombo vya habari nchini Tanzania, Membe amefariki akiwa katika hospitali Kairuki, Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Katika serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe alihudumu katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Mwaka 2007 hadi 2015.

Alipata umaarufu zaidi alipo chukua hatua ya kuwania urais mwaka 2020 ambapo aliamua kuhama chama tawala CCM na kujiunga na upinzani kupitia chama cha ACT wazalendo

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia ukurasa wake wa Twitter ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwanasiasa huyo nguli nchini Tanzania huku akisifu umahiri wake.

TRT Afrika