Mamo Mehretu Gavana wa Benki Kuu ya Ethiopia, NBE amesema hakuna sababu ya 'diaspora' kutuma pesa kupitia njia zisizo rasmi / Picha : NBE 

Benki 31 za Ethiopia zimezindua kampeni kubwa ya wananchi waishio nje yaani 'diaspora' kutuma pesa inayoitwa "DEBO," ambayo itakuwa kwa muda wa miezi sita ijayo.

Zaidi ya Waethiopia milioni 2.5 wanaishi nje ya nchi yao, hasa Marekani Kaskazini, Ulaya na Mashariki ya Kati, Uholanzi ikiwa mojawapo ya nchi zinazofikiwa miongoni mwa nchi nyingine.

Kampeni ya kutuma fedha itahusisha mpango kwa uratibu wa Benki Kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia, NBE).

"Hakuna sababu ya 'diaspora' kutuma pesa kupitia njia zisizo rasmi za hawala. Benki zetu zinatoa viwango bora zaidi kuliko soko haramu. Njia yetu ya kutuma pesa pia ni ya haraka na salama zaidi," amesema Gavana wa Benki Kuu ya Taifa ya Ethiopia, Mamo Mihretu.

Nia kuu ni kuwahimiza Waethiopia walio nje ya nchi kutuma fedha kupitia benki kwa kutoa viwango vya kuvutia vya kubadilisha fedha, kufungua akaunti kwa fedha za ndani au za kigeni, na kutumia fursa ya bidhaa mbalimbali za kuweka akiba na mikopo (kama vile rehani, mikopo, mikopo ya magari, na mikopo ya SME) inayohusishwa na utumaji fedha.

Benki zimetenga ETB bilioni 100 ( zaidi ya milioni $900 ) kwa madhumuni haya.

NBE pia imezindua jukwaa jipya la mitandao ambalo litawaruhusu Waethiopia na wageni wenye asili ya Ethiopia kufungua akaunti za benki nchini Ethiopia kwa karibu.

Mapato ya 'diapora' ya Ethiopia ni zaidi ya dola bilioni 5 katika fedha zinazotumwa kila mwaka, lakini serikali imegundua kuna mbinu za watu kutuma fedha kwa njia isiyo rasmi.

Kwa mfano, mtu aliye Marekani humpa mwenzake huko kiasi fulani cha fedha, na anayepewa anatoa maagizo kwa jamaa yake nchini Ethiopai kumpa jamaa wa yule mwengine fedha kiwango kile. Kwa njia hiyo, fedha hazipiti katika mifumo rasmi.

TRT Afrika