19 Machi mwaka 2024, Benki hiyo kubwa zaidi ya Ethiopia iliripotiwa kujaribu kurudisha fedha baada ya hitilafu ya kiufundi kuruhusu wateja kutoa zaidi ya walizokuwa nazo kwenye akaunti zao. / Picha: AFP

Benki ya Biashara ya Ethiopia imetangaza kuwa fedha ambazo zilitolewa na watu baada ya kuwepo kwa hitilafu katika mashine za ATM zimerudishwa.

"Hitilafu ya mfumo" wa hivi majuzi ulisababisha takriban zaidi ya dola milioni 14 kuwa hatarini kwa wizi. Zaidi ya wateja 25,000 walihusika katika kutoa pesa kupitia ATM na uhamisho wa kidijitali," Rais Abe Sano wa Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE) alitangaza.

19 Machi mwaka 2024, Benki hiyo kubwa zaidi ya Ethiopia iliripotiwa kujaribu kurejesha fedha baada ya hitilafu ya kiufundi kuruhusu wateja kutoa zaidi ya walizokuwa nazo kwenye akaunti zao.

Rais Sano wa Benki hiyo alisema kufikia Ijumaa CBE imepata asilimia 78 ya fedha zilizopotea, huku jitihada zikiendelea kurejesha zaidi ya dola milioni 2 zilizosalia zilizohamishiwa kwenye benki nyingine.

"Benki ilifanikiwa kurejesha zaidi ya dola milioni 2 kutoka kwa wateja walio na fedha za kutosha na zaidi ya dola 785,936 kutoka kwa wale ambao hawana salio la kutosha. Wakati wateja 9,281 kwa hiari walirudisha zaidi ya dola milioni 3.9.

Wateja 567 bado hawajarudisha zaidi ya dola172,694.

Benki inapanga kuchukua hatua za kisheria ikibidi.

Rais Abe alihakikisha kwamba CBE imejitolea kuhakikisha fedha zote zinarejeshwa na kuchunguza "hitilafu ya mfumo."

TRT Afrika