Sarafu mpya itakuwa na  utepe maalum wa usalama unaobadilika rangi kulingana na thamani ya noti./ Picha : Reuters 

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imetangaza uzinduzi wa sarafu mpya za noti zilizosasishwa.

Sarafu hii impya ina vitu vipya ndani yake mahsusi kwa ajili ya usalama.

Katika tangazo, lililochapishwa katika mitandao mbali mbali ya Benki Kuu ya Kenya , CBK ilisema noti hizo zitakuwa kwenye mzunguko sanjari na zile zilizopo sasa kwa maana kuwa kama mmiliki wa noti huna wasiwasi kufanya chochote kwa sasa au huna haja ya kukimbilia kubadilisha benki noti zako.

"Benki imefanya mabadiliko kadhaa katika baadhi ya sarafu za noti za shilingi mia moja (Sh100), shilingi mia mbili (Sh200), shilingi mia tano (Sh500) na noti za shilingi elfu moja (Sh1,000)," CBK ilisema Jumanne.

Mabadiliko hayo ni machache, ni si rahisi kuonekana wazi.

Vitu vipya vilivyotajwa ni :

Mwaka wa uchapishaji 2024 na sahihi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Chris Kiptoo.

Pia utepe maalum wa usalama unaobadilika rangi kulingana na thamani ya noti.

Benki Kuu ilisema itaanza kutoa noti hizo mpya kwanza kwa noti ya 1000, kisha zingine zitafuatia.

"Utoaji wa noti hizo utaanza na Sh1,000, huku sarafu zingine zitafuata taratibu ndani ya miezi ijayo," ilisema CBK.

Noti zilizoko kwenye mzunguko kwa sasa zilizinduliwa wakati wa sherehe za Siku ya Madaraka 2019, na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Mabadiliko mara kwa mara

Disemba 2018, Rais mstaafu Uhuru na aliyekuwa Gavana wa CBK Patrick Njoroge walizindua sarafu za kizazi kipya ambazo zinatumika kwa sasa.

Kubadilishwa kwa sarafu ya nchi huku Kenya ikiwa imefanya hivyo mara kadhaa wakati wa utawala wa Rais wa zamani, Daniel Arap Moi.

Mbali na kubadilisha muundo wa noti, Moi aliwahi kuleta sarafu mpya kabisa ikiwemo muundo mpya wa sarafu kama vile shilingi tano na kumi.

Vilevile, Kenya imeondoa mfumo wa kuweka picha za marais katika sarafu zake na badala yake huweka taswira kadhaa kama maliasili kama vile wanyama na milima.

TRT Afrika