Benki Kuu ya Kenya yaongeza kiwango cha riba / Picha: Reuters

Benki Kuu ya Kenya yaongeza kiwango cha riba kutoka 9.5% hadi 10.5%.

Gavana wa benki kuu ya Kenya Dkt. Kamau Thugge anasema hatua hiyo inalenga "kuimarisha matarajio ya mfumuko wa bei."

Uamuzi huo umefanywa licha ya ya tamko la kamati ya fedha nchini humo inayosema kuwa uchumi wa Kenya utaendelea kuimarika mwakani.

"Hii itatiliwa nguvu kwa upatikanaji wa sekta thabiti na maendeleo katika kilimo," alisema katika taarifa.

Kuongezeka kwa kiwango cha riba cha benki kuu tayari kumezua wasiwasi miongoni mwa wananchi hasa wale ambao wamechukua mikopo kutoka benki za biashara.

"Watu walio na mikopo wanapaswa kuulizia katika benki zao ili kufahamu athari za kupanda kwa kiwango cha riba katika benki," Polycup Osero, meneja wa maendeleo ya biashara wa Afrika Mashariki wa Software Group, anaiambia TRT Afrika.

Anasema kuongezeka kwa kiwango cha benki kuu kutaongeza moja kwa moja kiwango cha riba ambacho wakopaji wanapaswa kulipa kwa mikopo.

"Kuongezeka kwa kiwango cha Benki Kuu kunaweza kulazimisha benki za biashara pia kubana viwango vyao vya riba na hata kupunguza kiasi ambacho kinaweza kutolewa kwa mtu binafsi kwa ajili ya kukopa," Osero anaongeza.

Katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2023/2024 serikali inalenga kuongeza ufadhili wa ndani.

Rais William Ruto alitia saini kuwa sheria mswada wa Fedha wa 2023 ambao umeongeza wigo wa ushuru.

"Kupandisha viwango vya riba ya benki kunaweza kuifanya iwe vigumu kwa serikali kukusanya mapato kadri inavyotaka ndani," Osero anaongeza.

Benki kuu inasema akiba ya nje ya nchi kwa sasa inafikia dola milioni 7,379 ambayo ni miezi 4.07 ya malipo ya uagizaji.

Hii inasema itatoa kinga ya muda mfupi kwa uchumi wa nchi katika soko la fedha za kigeni.

TRT Afrika