Na Ramadhan Kibuga
TRT Afrika, Kinshasa, DRC
Jean Pierre BEMBA ametangaza kumuunga mkono Rais Felix Tchisekedi katika uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwaka huu .
Chama cha MLC'' Mouvement de Liberation du Congo'' cha Jean Pierre BEMBA kimetangaza uamzi wake huo baada ya kongamano la chama lilofanyika jumamosi hii Kinshassa.
Naibu huyo wa sasa wa Waziri Mkuu anayehusika na Ulinzi wa Taifa Jean Pierre Bemba ameahidi '' kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Rais aliye madarakani Felix Tshisekedi anashinda uchuguzi.''
Katika taarifa yake, Chama cha MLC kimekariri tena msimamo wake wa kubaki katika Muungano wa Vyama vinavyomuunga mkono Rais Tchisekedi '' Union Sacree de la Nation'' na Chama hicho kinasema kimeshuhudia wazi wazi azma ya Tchisekedi ya kuiwainua raia wa watu wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kufikia maendeleo na kuhakikisha uwepo usalama na amani ndani ya mipaka ya DRCongo.
''Ndio maana nimeamua kutogombea,'' amesema Jean Pierre Bemba mbele akihutubia wafuasi wa chama chake.
Kiongozi huyo wa Chama cha MLC amefafanua kwamba anataka kumuunga mkono Tchisekedi akimtaja kama ''ndugu'' na ''Rais wetu'' katika uchaguzi ujao ili '' aweze kuandaa mazingira mazuri ya Muungano wa Vyama ''Union Sacree'' na kufikia ushindi na hivyo kukamilisha kazi aliyoianzisha''
Jean Pierre BEMBA ana ushawishi mkubwa katika eneo lake la asili la Grand Equateur, Kaskazini Magharibi mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wadadisi wa siasa za Congo wanasema Tchisekedi atategemea saana eneo hili ili kushinda uchaguzi. Hivyo Tchisekedi atalazimika kushirikiana na baadhi ya viongozi wenye ushawishi katika maeneo mbalimbali ya DRC.
Katika Uchaguzi uliomalizika wa mwaka wa 2018 Jean Pierre BEMBA alimuunga mkono Kiongozi wa Upinzani Martin Fayulu ambae hadi sasa aliendelea kupinga matokeo ya uchaguzi.
Siku ya Jumamosi, Martin Fayulu alitangaza kwamba atakuwa mgombea kwenye uchaguzi wa urais wa tarehe 20 Disemba mwaka huu.