anga la Covid-19 lilifichua hali mbaya ya utengenezaji wa dawa barani Afrika, pamoja na ile ya chanjo/ Picha : X- Rais William Ruto

Viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Addis Ababa Ethiopia wameweka azimio la kujikimu kama bara katika utengenezaji wa chanjo kufikia mwaka 2040.

Hii ni kutokana na somo kali wanaosema wlaijifunza wakati wa janga la CVOID 19, ambapo Afrika ilionekana kubaguliwa katika utoaji wa chanjo.

Rais wa Kenya WIlliam Ruto aliyeongoza kamati ya viongozi juu ya chanjo, alisema wameafikiana kutafuta namna ya kujikimu ili kuondoa utegemezi wa magharibi katika suala la kufa kupona kama hilo.

''Janga la Covid-19 lilifichua hali mbaya ya utengenezaji wa dawa barani Afrika, pamoja na ile ya chanjo,'' alisema Rais Ruto katika mtandao wake wa X. ''Tulikuwa bara la mwisho kupata chanjo za Covid-19, na tuliteseka sana kutokana na 'utaifa wa chanjo','' aliongezea.

Tumejifunza na tumekoma

Rais Ruto, alielezea kuwa janga la COVID lilifichua kile ambacho kilikuwepo kimefichwa miaka mingi, kuwa kila mmoja ana maslahi ya watu wake kwanza kabla ya kuzingatia wengine, na Afrika inatakiwa kufuata mkondo.

''Lakini hali hii itabadilika kuwa bora. AU imeazimia kuwa ifikapo mwaka 2040, asilimia 60 ya chanjo zinazotumika barani Afrika zitazalishwa nchini humo,'' aliendelea kusema Rais Ruto.

Tangazo hili linaendana na Ushirikiano wa Utengenezaji Chanjo wa Kiafrika (PAVM) ulioundwa ili kuimarisha mfumo ikolojia wa utengenezaji wa chanjo wa Kiafrika kufikia mwaka 2040.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya kudhibiti magonjwa Afrika (ACDC), uwezo wa kutengeneza chanjo wa Kiafrika umejikita zaidi kwenye mfumo wa kutengeneza, kujaza na kumaliza chanjo yote, huku kiwango kikubwa cha uwezo wa ziada bado kikiwa katika awamu ya mipango.

Kuna uhamishaji wa teknolojia duni unaotumika kusaidia idadi kubwa ya uwezo wa sasa wa utengenezaji chanjo. / Picha : X- William Ruto 

Africa CDC inahofia kuwa iwapo mipango yote itatekelezwa, uwezo wa kuunda, kujaza na kumaliza chanjo ungekuwa zaidi ya maradufu ya makadirio ya mahitaji ya chanjo ya Kiafrika mwaka wa 2030. Katika kiwango hicho cha uwezo, kuna hatari sio kila mradi wa utengenezaji ungekuwa endelevu na wa kibiashara.

Hata hivyo wataalamu wanashauri kufanywa utafiti zaidi kupata taswira halisi ya mapungufu na mahitaji katika mfumo ikolojia wa utengenezaji wa chanjo ili kuhakikisha washikadau wote pania kusonga mbele na miradi mipya na uwekezaji.

PAVM inalenga kuanzisha vituo vitano vya utafiti na utengenezaji wa chanjo katika bara katika kipindi cha miaka 10-15 ijayo, na kuongeza sehemu ya chanjo zinazozalishwa barani kwa ajili ya matumizi ya bara hilo hadi 60%.

Ustawi wa mauzo ya chanjo barani

Tayari mataifa kadhaa ya Afrika yamewekeza katika utengenezaji wa chanjo kupitia ufadhili wa kifedha na kimkakati kutoka kwa taasisi ya chanjo barani Afrika MAV, ikiwemo Kenya, Morocco, Afrika Kusini, Nigeria na Ghana.

Africa CDC imeelezea changa moto kubwa inayokabili Afrika ni iutegemezi wa bara kwa uhamishaji wa teknolojia kutoka kwa watengenezaji wa chanjo wasio Waafrika.

Lakini kuna uhamishaji wa teknolojia duni unaotumika kusaidia idadi kubwa ya uwezo wa sasa na uliopangwa wa utengenezaji wa chanjo.

Utafiti pia ulihitimisha kuwa baadhi ya watengenezaji chanjo wa Kiafrika tayari wana uwezo mkubwa wa kifedha (njia za kupata ufadhili wa vifaa na shughuli zinazohitajika kuzalisha chanjo) lakini wanahitaji kukuza zaidi uwezo wao wa kibiashara.

Miongoni mwa mapendekezo kuhusu njia ambazo watengenezaji chanjo wa Kiafrika wanaweza kuboresha uwezekano wao wa kufaulu ni pamoja na kuzingatia chanjo ambazo zina uwezo mkubwa wa soko na kuimarisha mipango ya biashara.

TRT Afrika