Mwanamke wa Afrika Kusini (Kushoto) ambaye wengi wanasema amefanana na Oprah Winfrey (Kulia).

Na Pauline Odhiambo

Mara nyingi wao inasemekana kuwa kila mtu ana watu saba anaofanana nao kote duniani. Lakini utafiti unaonesha uwezekano wa watu wawili kuwa na ishara nane za kufanana usoni ni nadra sana.

Kulingana na utafiti katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, licha ya hali hii ya kushangaza, wapo watu ambao wanafanana na mara nyingi wanaishi sehemu tofauti ya dunia.

'Pacha' wako ina maana mtu ambaye anafanana na wewe na hana uhusiano wowote na wewe. Mara nyingi si rahisi kwa watu hawa kuonana ana kwa ana na huwa hata hawajuani hadi pale itakapotokea fursa ya aina yake, au labda mitandao ya kijamii iwalete pamoja.

Hili ndilo lililotokea kwa mwanamke mmoja Afrika Kusini ambaye alikuwa maarufu mitandaoni baada ya picha yake kuwepo katika mitandao kadhaa.

Mwanamke anayefanana na Oprah Winfrey nchini Afrika Kusini.

Is that you, Oprah?

Katika picha, mwanamke huyo ambaye bado hajatambuliwa anaonekana ameshika kikaratasi cha moja ya maduka makubwa, lakini kilichowashangaza wengi ni namna mwanamke huyo alivyofanana na tajiri mmiliki wa chombo cha habari wa Marekani Oprah Winfrey.

Raia wa Afrika Kusini walitambuwa namna mwanamke huyo alivyofanana na mtu huyo maarufu wakisema kuwa 'ni pacha wa Oprah aliyepotea.’

Mtumiaji wa mtandao wa Facebook Jan Van Potgieter, ambaye ndiye wa kwanza kuweka picha hiyo kwenye ukurasa wake, aliandika: “Oprah Winfrey ashinda vocha ya duka la Shoprite.”

Wakijibu alichoandika Potgieter, wengine walikuwa na maneno kadhaa ya ucheshi wakimfananisha na namna Oprah alivyokuwepo kwenye televisheni.

Wakikumbuka wakati mmoja ambapo kila aliyekuja kwenye kipindi chake alipewa zawadi ya gari, mtu mmoja aliandika, “Yay, unapata vocha, unapata vocha, kila mtu atapata vocha ya Shoprite!”

“Huyu ni Opra Winfried kutoka Temu,” ujumbe mwingine ulisema, kuzungumzia uuzaji bidhaa wa mitandaoni kwa bei nafuu zaidi.

Wanaofanana na watu maarufu

Pamoja na kuwa watu maarufu ni miongoni mwa wale wanaofahamika zaidi duniani, na ambao sura zao zinaonekana kwenye matangazo mbali mbali, baadhi ya watu hufananishwa na watu maarufu zaidi duniani.

DJ na mtayarishaji wa muziki wa Afrika Kusini Black Coffee alishangaa alipomuona 'pacha' Real Phumzo, katika sehemu moja ya burudani mjini Cape Town.

Vile vile, mtayarishaji wa muziki kutoka Eswatini Uncle Waffles na mwanamuziki wa Afrika Kusini singer Seemah walikutana baada ya mashabiki kusema kuwa ni 'mapacha' waliopoteana.

Hawa hawa ni baadhi ya watu maarufu ambao wanafanana.

Rihanna na Priscila Beatrice

Nyota wa TikTok mwenye umri wa miaka ishrini na nane Priscila Beatrice amefanana na mwanamuziki maarufu Rihanna, kiasi cha Rihanna kuzungumzia ubunifu wake uliofanya watu wadhani kuwa ni yeye.

Akizungumzia kuhusu ubunifu huo wa Beatrice, mwanamuziki huyo wa ‘Work’ aliandika: “albamu iko wapi dada? #R9”, kwa mzaha akimzungumzia Priscila na tasnia ya muziki.

Beyoncé (Kushoto) na anayefanana naye Brittany ‘SurB’ Williams.

Beyoncé na Brittany ‘SurB’ Williams

Brittany Williams, mwenyeji wa Detroit, inasemekana amekuwa akikabiliana na hali hii ya kufananishwa na Malkia Bey kwa miaka mingi. Kulingana na gazeti la 'The Daily Mail', mara kwa mara anasimamishwa barabarani na mashabiki wa mwanamuziki huyo wa wimbo wa ‘Drunk In Love’.

“Kila mara watu wananiuliza; kwenye ndege, uwanja wa ndege au wakati ninapokuwa kwenye hafla mbali mbali. Pia kuna watu wananifuata kunipiga picha bila ridhaa yangu na kunifanyia mizaha bila mimi kujua,” aliliambia gazeti hilo2017.

“Kundi moja la wanawake lilitufuata mimi na rafiki yangu hadi kwenye gari letu na kuanza kuimba wimbo wa ‘Single Ladies’, wakigonga gari kwa viatu vyao mpaka tukashusha vioo vya gari na kupiga nao picha.”

Meghan Markle (Kushoto) na Akeisha Varnado Land.

Meghan Markle na Akeisha Land

Wakati nyota wa mtandaoa wa Instagram Akeisha Varnado Land alipoweka picha yake na ya binti yake Februari 2020, hakuwa amejiandaa kwa namna watu walivyozungumzia kufanana kwake na Meghan Markle, bintimfalme wa Sussex.

“Watu wananifananisha na yeye sana, na siyo mitandaoni pekee. Hata wakati nikiwa natembea, nikiwa kanisani, maeneo ya kutizama filamu, au hata dukani kununua bidhaa… hata marafiki zangu wa karibu na jamaa zangu wanasema nimefanana naye! Pamoja na kuwa mimi mwenyewe sioni tumefanana vipi, kwa kweli nachukulia kama jambo zuri,” Mmarekani huyo aliliambia gazeti la The Daily Mail.

“Mara nyingi mimi hutania nikisema kama kuna mtu wake wa karibu amwambie niko tayari kwenda kwenye hafla ambayo amealikwa na hataki kwenda mimi niende kama 'pacha' wake.”

TRT Afrika