Marekani inachukizwa na baadhi ya chaguzi za sera za kigeni za Afrika Kusini ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kuipeleka Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu mauaji ya halaiki huko Gaza. /Picha: TRT Afrika

Na Millicent Akeyo na Sylvia Chebet

Afrika Kusini inakabiliwa na kile inachokiona kama uonevu unaofanywa na Marekani baada ya Rais Donald Trump kufungua tena jeraha la zamani kwa kutilia shaka sheria mpya ya unyakuzi wa ardhi ya nchi hiyo.

"Mambo mabaya yanatokea Afrika Kusini," Trump alidai hivi majuzi. "Wanachukua ardhi, wananyang'anya ardhi, na kwa kweli wanafanya mambo ambayo labda ni mabaya zaidi kuliko hayo."

Afrika Kusini ilijibu kwa ukali madai hayo. "Hatutaonewa," alisema Rais Cyril Ramaphosa.

Msemaji wa rais, Vincent Magwenya, alifafanua kuwa Afrika Kusini haina sheria ya umiliki wa kibaguzi.

"Sheria zetu zote zinatokana na Katiba yetu," alisema, akisisitiza kuwa sheria ya unyakuzi wa ardhi ilikusudiwa kushughulikia tofauti za kihistoria za kikabila badala ya kutumika kama chombo cha unyakuzi.

Makosa ya kihistoria

Umiliki wa ardhi nchini Afrika Kusini unabeba kumkumbu za huzuni.

Mnamo 1913, watawala wa kikoloni wa Uingereza walipiga marufuku watu weusi nchini Afrika Kusini kumiliki au kukodisha ardhi kama sehemu ya sera zao za kuwanyima watu na kuwatenga.

Kama Wakili Tembeka Ngcukaitobi anavyosema, "Ubaguzi wa rangi haukuwa tu mfumo wa kisiasa, pia ulikuwa mfumo wa kiuchumi, na ulijenga uchumi wa aina yake kwa kuwafungia watu weusi wasishiriki."

Takwimu zinaonyesha ukweli huu chungu. Wakulima wa kizungu, ambao ni asilimia 8 tu ya watu milioni 63 wa Afrika Kusini, wanamiliki takriban robo tatu ya ardhi ya nchi hiyo.

Hili halijabadilika sana tangu ubaguzi wa rangi ulipomalizika rasmi mwaka wa 1994.

Januari hii, Rais Ramaphosa alitia saini Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi ambayo inaipa serikali mamlaka ya kuchukua ardhi ya kibinafsi - ikiwa ni pamoja na kutolipa fidia ya fedha - ikiwa zoezi hilo litazingatiwa "haki na usawa na kwa maslahi ya umma".

Msomi na mtaalamu wa mikakati Ongema Mtimka anaamini kuwa Trump alikosea alipochagua Afrika Kusini. Anaamini kuwa hii sio chochote zaidi ya siasa.

"Ni wazi kabisa kwamba Trump anacheza karata ya diplomasia ya kulazimisha, ambayo Marekani imecheza katika historia inapokuja kwa serikali ambazo hazifanyi kazi zake katika sera ya kigeni," anaiambia TRT Afrika.

"Tunafahamu kuwa Afrika Kusini imekuwa na chaguzi za sera za kigeni ambazo hazikupendelewa na Marekani katika miaka ya hivi karibuni, kuanzia vita vya Urusi na Ukraine, kuipeleka Israeli katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, pamoja na ushiriki wake katika BRICS. Yote haya yanaonekana na utawala wa Trump kama ushirikiano usioendana na siasa za Marekani."

Sheria yenye utata

Ingawa sheria mpya imeundwa kutekeleza madhumuni mahususi, maoni yamegawanyika ndani ya Afrika Kusini kuhusu dhamira na utekelezaji wa serikali.

Kallie Kriel, anayeongoza shirika lisilo la kiserikali la AfriForum ambalo linazungumza zaidi na Waafrikana anasema hatua za Trump zilitarajiwa kufuatia kupitishwa kwa sera mpya ya ardhi.

"Sio lazima uwe mwanauchumi kujua kwamba ukivunja haki ya kumiliki mali, itawatia hofu wawekezaji. Itajenga maadui katika nchi ambazo zina hisia kali kuhusu soko huria. Na hivyo ndivyo ilivyotokea wakati Rais Ramaphosa aliposaini Sheria ya Unyakuzi," anasema.

Kiongozi wa Upinzani wa Afrika Kusini, John Hlophe wa Chama cha MK, anaishutumu AfriForum kwa kuharibu maslahi ya nchi kwa kueneza habari za uongo nje ya nchi.

"Uhaini umefanywa...wanapanga njama dhidi ya serikali yetu," anasema.

"Kwanza kabisa, walidanganya na kusema mashamba yao yametwaliwa...kumekuwa na mauaji, na ardhi yao ilitwaliwa, jambo ambalo si kweli. Kwa hiyo, kwa kuzingatia uwongo huo na upotoshaji wa ulaghai, Trump alitoa amri ya rais dhidi ya Afrika Kusini."

Suala la hadhi ya ukimbizi

Kando na kutishia kuinyima msaada Afrika Kusini, utawala wa Trump unapendekeza kuwapa hadhi ya ukimbizi Waafrika Kusini weupe nchini Marekani.

Majibu kutoka kwa makundi yanayowakilisha wazungu wachache nchini Afrika Kusini kwa Trump yamekuwa, "Asante, lakini hatutaki."

Harakati ya Orania Movement ambayo inatetea haki ya kujitawala kwa Waafrikana, inaona msimamo wa Waamerika kuhusu suala hilo kama kujidhalilisha bila sababu.

"Mtazamo wetu kwa hili uko wazi sana," imeiambia TRT Afrika. "Tunaamini Waafrika ni wazawa barani Afrika; sisi ni wa Afrika. Hatutaki kuwa kikundi cha wachache wanaolindwa au kuwa wakimbizi katika nchi ya mtu mwingine."

Kriel wa AfriForum anakataa wazo la hadhi ya ukimbizi nchini Marekani kwa Waafrika Kusini weupe.

"Hatutaki kuhamia kwingine. Hatutawaomba watoto wetu sasa wahamie nchi nyingine. Ukweli ni kwamba, mababu zetu walijitahidi sana kuhakikisha kwamba sisi kama watu tunaunda ncha ya kusini mwa Afrika. Hatutadharau hilo."

Viwimbi mahali penginePamoja na ukosoaji wa Trump kwa Afrika Kusini kuibua hisia za kimataifa, mchakato wa mageuzi ya ardhi unatazamwa kwa karibu na mataifa mengine yanayokabiliana na ukosefu wa usawa wa kihistoria.Serikali inasisitiza kuwa sheria mpya inaambatana na viwango vya kimataifa vya haki za kumiliki mali huku ikishughulikia changamoto za kipekee za ndani."Tutazungumza kwa sauti moja kutetea maslahi yetu ya kitaifa, mamlaka yetu na demokrasia yetu ya kikatiba. Kwa kusimama waaminifu kwa maadili yetu, kutumia uwezo wetu wa kipekee na wakfu, na kuunda madhumuni ya pamoja, tunaweza kubadilisha mazingira haya ya majaribio kwa manufaa yetu," Rais Ramaphosa alisema katika taarifa yake rasmi.Wengine wanaweza kusema ukosoaji wa Trump unaweza kufanya kile ambacho miaka ya kazi ya upatanisho haikuweza - kuwaunganisha Waafrika Kusini kulinda maslahi yao ya pamoja ya kitaifa.Huku Afrika Kusini ikipitia mchanganyiko huu wa mateso ya zamani na siasa mpya, ulimwengu unatazama kuona kama kurekebisha umiliki wa ardhi kunaweza kuponya yaliyopita bila kuunda majeraha mapya.

Ulimwengu unatazama

Pamoja na ukosoaji wa Trump kwa Afrika Kusini kuibua hisia za kimataifa, mchakato wa mageuzi ya ardhi unatazamwa kwa karibu na mataifa mengine yanayokabiliana na ukosefu wa usawa wa kihistoria.

Serikali inasisitiza kuwa sheria mpya inaambatana na viwango vya kimataifa vya haki za kumiliki mali huku ikishughulikia changamoto za kipekee za ndani.

"Tutazungumza kwa sauti moja kutetea maslahi yetu ya kitaifa, mamlaka yetu na demokrasia yetu ya kikatiba. Kwa kusimama waaminifu kwa maadili yetu, kutumia uwezo wetu wa kipekee, na kujitegema na vile vile kuunda madhumuni ya pamoja, tunaweza kubadilisha mazingira haya ya majaribio kwa manufaa yetu," Rais Ramaphosa alisema katika taarifa yake rasmi.

Wengine wanaweza kusema ukosoaji wa Trump unaweza kufanya kile ambacho miaka ya kazi ya upatanisho haikuweza - kuwaunganisha Waafrika Kusini kulinda maslahi yao ya pamoja ya kitaifa.

Huku Afrika Kusini ikipitia mchanganyiko huu wa mateso ya zamani na siasa mpya, ulimwengu unatazama kuona kama kurekebisha umiliki wa ardhi kunaweza kuponya yaliyopita bila kuunda majeraha mapya.

TRT Afrika