Afrika Kusini imetangaza kinga ya kidiplomasia kwa watu ambao watahudhuria mikutano miwili ya BRICS iliyopangwa mwaka huu nchini Afrika Kusini.
BRICS ni muungano wa nchi tano kwa ajili ya kujiendeleza: Brazil, Urusi, Uchina India na Afrika Kusini.
Kinga hii ambayo imetolewa kupitia taarifa rasmi ya serikali yaani gazette, inamaanisha wajumbe wa Urusi hawatakamatwa wakiwa nchini humo watakapohudhuria mkutano wa mawaziri wa muungano wa BRICS, kati ya tarehe 1 na 2 mwezi Juni mwaka huu, mjini CapeTown nchini humo.
Amri hii imetiwa saini na Waziri wa Mahusiano ya kimataifa na ushirikiano.
Itawakinga wajumbe watakaohudhuria mkutano wa marais wa muungano wa BRICS unaotarajiwa kati tarehe 22 na 24 Agosti 2023, jijini Johannesburg nchini humo.
Inamaanisha kuwa rais wa Urusi, Vladimir Putin, anaweza kuhudhuria mkutano huo wa Agosti bila hofu ya kukamatwa.
Brazil , Urusi , Uchina na India ziliunda muungano huu wa BRICS wa kiuchumi Juni mwaka 2009. Afrika Kusini baadaye ilialikwa kujiunga nao Desemba 2010.