Ziwa maarufu kama ‘Pink lac’ nchini Senegal ni mojawapo ya chanzo cha zaidi tani 500,000 ya chumvi ambayo Senegal / Picha: AFP

Na Coletta Wanjohi

Istanbul, Uturuki

Ziwa hili maarufu kama ‘Pink lac’ nchini Senegal ni mojawapo ya chanzo cha zaidi tani 500,000 ya chumvi ambayo Senegal inazalisha kwa mwaka na kuifanya kuwa nchi yenye uzalishaji mkubwa wa chumvi magharibi mwa Afrika.

Inafuatiwa na Ghana ambayo inatoa takribani tani 300,000 ya chumvi huku nchi nyengine kama Togo zikifuata.

Huko Kusini mwa Afrika, Namibia inaongoza kwa kuzalisha zaidi ya tani 900,000 ya chumvi huku Afrika Kusini ikitoa Zaidi ya 300,000 kila mwaka.

Huko Kaskazini, Misri inazalishwa zaidi ya tani milioni mbili ya chumvi na Tunisia ikitoa zaidi ya tani milioni 1.5 ya chumvi kila mwaka.

Nchi zetu za Afrika Mashariki pia zina akiba kubwa ya chumvi. Tanzania ikizalisha zaidi ya tani 182,000 ya chumvi, huku Kenya ikiripotiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 850,000 ya chumvi kwa mwaka.

Takwimu zinaonyesha kuwa mahitaji ya chumvi barani Afrika ni takribani tani milioni 7 kwa mwaka/ Picha : Getty 

Hata hivyo, uzalishaji wake ni asilimia 60 tu. Huu ni ni utajiri mkubwa wa bara la Afrika.

Takwimu zinaonyesha kuwa mahitaji ya chumvi barani Afrika ni takribani tani milioni 7 kwa mwaka.

60% ya chumvi Afrika inatumika katika usindikaji wa chakula, huku nyengine ikitumika katika utengenezaji wa kemikali, na matibabu ya maji.

Bei ya chumvi ya bara ni kati ya dola 30 hadi 60 kwa tani moja, ikitofautiana na nchi tofauti.

Misri inauza nje karibu 30% ya uzalishaji wake wa chumvi, haswa kwa nchi za Ulaya na Asia. Senegal nayo inauza takriban tani 150,000 za chumvi kila mwaka, kwa nchi za Afrika Magharibi.

Licha ya uzalishaji mkubwa wa chumvi barani Afrika, bado Afrika inapata chumvi kutoka nje ya bara.UAE, Uchina na Spain zinatoa ushindani mkubwa wa biashara ya chumvi Afrika.

Uzalishaji wa chumvi afriak unafanya na wakulima wadogo wadogo / picha: AFP

Wataalamu wa masuala ya biashara wanasema hii imechangiwa na uwekezaji mdogo katika viwanda vya chumvi hasa usindikaji na kuongeza thamani. Asilimia kubwa ya uzalishaji Afrika, ni wa kiwango cha chini unaofanywa na watu binafsi.

Mathalan, nchini Uganda, wakazi wa Ziwa Katwe inazalishwa chumvi, wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu ukosefu wa vifaa vya kujikinga pindi wanapoingia ziwani kuvuna chumvi.

Malalamiko hayo yamesikika zaidi kutoka kwa wanaume, ambao wanadai kupata athari za kiafya.

Bei ya chumvi ya bara ni kati ya dola 30 hadi 60 kwa tani moja, ikitofautiana na nchi tofauti/ Picha: Reuters 

Wakati huo huo, soko la chumvi duniani linazidi kuongezeka, inaongezeaka huku viwanda vya chakula, kuoka ngozi, kupaka rangi, na kutengeneza vyombo vya udongo, sabuni na klorini bado vinaendelea kupanuka.

Ili kunufaika na upanuzi wa soko la chumvi, Afrika inatakiwa kuipa sekta hii kipaumbele kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoinua thamani na kiwango cha chumvi.

TRT Afrika