Jeshi la polisi limetahadharisha watu kusambaza zaidi video hiyo, au kutoa maelezo ya uongo juu yake./ Picha : X- Jeshil a polisi Tanzania

Jeshi la polisi nchini Tanzania limetangaza kuwakamata washukiwa wanne kuhusiana na kisa cha ubakali na udhalilishaji uliofanywa dhidi ya msichana mmoja katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Polis iwanasema wamefuatilia video iliyosambazwa mtandaoni kuwasaka wahalifu pamoja na wale waliohusika katika kusamabaza video hiyo ambayo alisema inaonyesha udhalilishaji wa hali ya juu wa binadamu.

Baadhi ya watuhumiwa hao wamekamatwa mkoani Dodoma na mkoa wa Pwani kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi.

''Uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata binti aliyefanyiwa ukatili huo na amehifadhiwa eneo salama na anaendelea kupata huduma zinazostahili kupewa mtu aliyefaniwa ukatili wa aina hiyo,'' alisema David Misime, Msemaji wa Jehsi la Polisi, Dodoma Tanzania.

Polisi pia wametoa onyo kwa wanachi wanaojitokeza nyumbani kwa binti huyo na familia yake kuwahoji au kuwatazama akisema ni ukiukaji w ahaki yao ya faragha.

Katika onyo nyingine waliotoa polisi kwa wananchi ni kuwa watakaohujumu kukamatwa kwa washukiwa wengine wawili ambao walihusika na ubakajina bado wanasakwa pia watafunguliwa mashtaka.

Polisi wamewataka raia kutoa maelezo yoyote watakuwa nayo juu ya waliko washukiwa.

Mnamo Agosti 2 2024, video ilianza kusambaa mtandaoni ikimuonyesha binti mmoja akibakwa na genge la majambazi huku wakimdhalilisha kinyume cha maumbile.

Video hiyo imesababihsa ghadhabu kubwa miongoni mwa wananchi wa Tanzania na nje, wakitaka polisi kuwachukukia hatua kali wahusika.

Polisi bado wanaendelea na uchunguzi zaidi japo kumekuwa na maelezo yasiyothibitishwa juu ya mazingira ya kutokea uhalifu huo pamoja na kuchukuliwa video.

Jeshi la polisi limetahadharisha watu kusambaza zaidi video hiyo, au kutoa maelezo ya uongo juu yake.

''Watuhumiwa wanne wamkamatwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza taarifa za uongo mitandaoni zinazosema RIP binti aliyebakwa...'' alisema Misime katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. ''Taarifa zingine za uongo zimesema kuwa binti huyo amefariki.'' aliongeza Misime, akionya kuwa wenigne watakaosambaza taarifa za uongo kuhusiana nakisa hicho watakamatwa.

Washukiwa wawili waliohusika katika ubakaji na upangaji wa uhalifu huo wanasakwa bado.

TRT Afrika