Takriban watu wawili walifariki Jumanne asubuhi katika ajali iliyohusisha magari mengi kwenye barabara ya Southern Bypass, jijini Nairobi.
Wengine watatu walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ya Jumanne alfajiri asubuhi iliyotokea karibu na eneo la Ole Sereni, katika barabara kuu ya kuunganisha mtaa wa Langata na barabara ya kwenda Mombasa road, inayopita karibu na uwanja wa ndege wa JKIA .
''Watu watatu wamepelekwa hospitalini, kutokana na juhudi za timu ya mashirika mbalimbali ya kukabiliana na hali hiyo,'' iliandika shirika la msalaba Mwenkundu la Kenya katika mtandao wa X.
Red cross inasema magari matatu yalihusika katika ajali hiyo.
Kwa mujinbu wa walioshuhudia, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa lori lililokuwa likitoka upande wa Kikuyu, kushindwa kulimudu, na kuacha njia yake na kuvuka kuelekea upande wa pili na kugongana na trela.
''Kulitokea mlipuko na moto kuwaka uliofok amoshi mkubwa kufuatia mgongano huo,'' Red cross ilisema.
Idara ya polisi inasema kuwa madereva wote wawili walifariki papo hapo, huku mmoja wao akiteketea kiasi cha kutotambulika.
Wasamaria wema walijitolea kuwasaidia baadhi ya abiria waliokuwa wamenaswa kwenye magari hayo.
"Tunachunguza jinsi na kwa nini ilifanyika," alisema DktResla Onyango, msemaji wa Polisi wa Kitaifa.
Mamlaka ya usalama wa barabarani nchini Kenya inakadiria kuwa zaidi ya watu 4000 hufariki katika ajali za barabarani kila mwaka, huku nyingi ya ajali hizo zikisemekana kusababishwa na tairi mbovu kupasuka, dereva kushindwa kudhibiti vyombo hasa pikipiki na malori na nyingine.