Picha ya satellite inaonyesha gati ya Marekani ikielea kwenye pwani ya Gaza, Mei 26, 2024. / Picha: Reuters

Na

Nadia Ahmad

Juhudi za Marekani za kuwapa Wapalestina misaada ya kibinadamu kupitia gati iliyojengwa hivi karibuni katika pwani ya Gaza haziendi vyema. Mradi huo wenye thamani ya dola milioni 320, ambao ulichukua miezi miwili kujengwa, ulifanya kazi kwa wiki moja tu mwezi Mei, kabla ya kusambaratika kutokana na hali mbaya ya hewa. Sasa unafanyiwa matengenezo.

Kutoa misaada ya kibinadamu kwa Gaza iliyoharibiwa na Israeli inaonekana kuwa jambo jema sana. Hata hivyo, uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kuwa nia potofu zinatumika ambazo zinaweza kuharibu zaidi eneo hili na kuunda upya mazingira ya nishati kwa ajili ya maslahi ya kampuni ya Marekani.

Kwa kuzingatia historia ya sekta ya mafuta na gesi, gati hio ya Marekani inaweza kuwa udanganyifu, kuficha mipango ambayo itazidisha migogoro na kukosekana usawa.

Gati hio huenda ikawa ni kisingizio cha Marekani inayolingana na ajenda yake fiche, hasa pale ambapo kunapitikana mafuta na gesi. Hii ni pamoja na kuongezeka kwa mvutano wa kisiasa wa kijiografia kati ya Ekuado na Meksiko na kati ya Guyana na Venezuela.

Uwepo wa kijeshi wa Marekani

Gati la Gaza pia linaongeza rekodi ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken katika kuchochea vita kutumia jina la diplomasia. Licha ya ahadi za kumaliza "vita vya milele" na kutetea haki za binadamu, hatua chache zimechukuliwa hadi sasa.

Ufanisi wa gati hilo katika kupunguza kwa kiasi kikubwa mzozo wa kibinadamu wa Gaza unatia shaka. Misaada mingi inapita kwenye vivuko vya mpaka, na vizuizi vya Israeli katika maeneo haya bado vinaendelea, na kuzuia harakati na ufikiaji wa mahitaji ya kimsingi.

Jambo la kutilia shaka zaidi ni uwepo wa wanajeshi wa Marekani na athari za mikataba ya kikanda ya gesi.

Kutumwa kwa wanajeshi 1,000 wa ziada wa Kimarekani, wanaoonekana kusaidia katika juhudi za misaada, inaongeza shaka kutokana na uungaji mkono mkubwa wa kijeshi wa Marekani kwa Israeli. Kuimarishwa huku kwa vikosi karibu na Gaza kunaweza kuwa ni jaribio la kuendeleza maslahi ya kimkakati ya Marekani na Israeli, ikiwa ni pamoja na kutumia hifadhi ya gesi iliomo baharini ambayo haijatumiwa.

Hii inaweza kuwa kweli hasa kwa kampuni ya Chevron, ambayo imehusika katika utafutaji wa gesi katika pwani ya Israeli na imeshirikiana na makampuni ya Israeli katika miradi mikubwa.

Wakati Rais Donald Trump alimteua Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa ExxonMobil Rex Tillerson kama Waziri wake wa kwanza, Biden amemwamini Blinken, ambaye hapo awali alikuwa mshauri wa Chevron, kwa ustadi wake katika diplomasia ya nishati.

Pamoja na safari 75 za kustaajabisha kwa nchi 84 kufikia mwisho wa mwezi uliopita, Blinken anaonyesha uwezo wa mwanadiplomasia aliyebobea. Mtindo wake wa hali ya juu, vipengele vilivyosawazishwa, na kutegemewa kwa mradi wa mawasiliano wazi, kukuza uaminifu, na kuwezesha ushiriki wa kimataifa.

Ingawaje uhalisia wa mambo kuna ushawishi wa mashirika makubwa ya kimataifa na hamu yao isiyoweza kutoshelezwa ya mafuta na gesi.

Wakati ndege ya Blinken ikitanda kote duniani, hatua zake zinaakisi utawala wa Marekani unaotanguliza maslahi ya mashirika badala ya haki za binadamu, huku ukifumbia macho mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza. Iwapo Blinken kweli ana nia ya kusitisha vita angekuwa amefanya hivyo.

Hisa za Chevron

Gati la Gaza, na kuongezeka kwa uwepo wa jeshi la Merikani, kunaweza kufungua njia kwa Chevron kutawala eneo hilo la bahari ya Gaza, na kuharibu mazingira na haki za ardhi za Wapalestina.

Udhibiti wa hifadhi hizi za gesi ungebadilisha kwa kiasi kikubwa uwiano wa kikanda wa nguvu na kampuni za nishati za Chevron na Marekani zinazoelekea kufaidika, huku ukiongeza mivutano kuhusu rasilimali. Kuruhusu Israel kupanua wigo wake wa nishati na Marekani kupanua chapa yake ni kinyume na maslahi ya muda mrefu ya kiuchumi na kimkakati ya mataifa ya kikanda.

Udhibiti wa hifadhi hizi za gesi una uwezo mkubwa wa kubadilisha kwa kiasi kikubwa usawa wa nguvu za kikanda huku kampuni za nishati za Chevron na Marekani kuelekea kufaidika, na kuongeza mivutano kuhusu rasilimali. Kuruhusu Israeli kupanua wigo wake wa nishati na Marekani kufaidika ni kinyume na maslahi ya muda mrefu ya kiuchumi na kimkakati ya mataifa ya kikanda.

Chevron ina historia ya kuingilia kesi za kimazingira na uingiliaji kati wa haki za binadamu, hasa pale ambapo mafuta na gesi inahusika.

Mara tu baada ya Biden kuchukua madaraka mnamo Februari 2021, jeshi la Myanmar lilipindua serikali yake iliyochaguliwa kidemokrasia. Chevron, ambayo ilikuwa na uhusiano wa muda mrefu na kampuni inayomilikiwa na serikali iliyounganishwa na majenerali wa kijeshi, ilifanikiwa kushawishi dhidi ya vikwazo ambavyo vingevuruga shughuli za jeshi.

Kama mfano mwingine, Chevron ilikwepa hukumu ya dola bilioni 9.5 dhidi yake nchini Ecuador kwa uchafuzi wa mafuta kwa kufungua kesi ya RICO dhidi ya wakili Steven Donzinger. Jaji wa Manhattan alibatilisha Mahakama ya Juu ya Ecuador, na kufanya uamuzi huo kutotekelezeka.

Mapema mwaka huu. Katika Kongamano la Kiuchumi Duniani la mwaka 2024, Blinken alijadili athari za vita zinazoweza kutokea huko Gaza na mabadiliko ya kihistoria katika Mashariki ya Kati, akisisitiza ulazima wa kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina. Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Chevron Michael Wirth alielezea wasiwasi kuhusu hatari kwa usafirishaji wa mafuta na uwezekano wa kuongezeka kwa bei.

Kusitasita kwa utawala wa Biden kuingilia kati masuala ya haki za binadamu nchini Myanmar na Israeli, pamoja na kuwepo kwa wafanyakazi wa zamani wa WestExec Advisors katika nyadhifa muhimu, kunaibua wasiwasi kuhusu kuweka kipaumbele kwa maslahi ya shirika kuliko haki za binadamu.

Mfano uliowekwa hapo awali na Chevron, linapokuja suala la kuweka kipaumbele masilahi ya mafuta, unapendekeza kwamba ushawishi wa kampuni ndani ya utawala unaweza kuwa uliunda maamuzi ya sera ya kigeni kwa njia ambayo ilinufaisha kampuni hio.

Jibu la Mashariki ya Kati

Katika kukabiliana na matukio haya, nchi za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika lazima zichukue hatua madhubuti, kukabiliana na hatua za Marekani na Israeli. Kizuizi cha mafuta kinacholenga Israeli kinaweza kuwa kifaa chenye nguvu, kikiwagonga pale inapoumiza kiuchumi.

Nchi hizo pia zinapaswa kufikiria kuiwekea Israeli vikwazo ili kuishinikiza kukomesha mzingiro wa Gaza na kukomesha unyonyaji wa rasilimali za Wapalestina.

Huku uchaguzi wa urais wa Marekani ukikaribia kwa kasi, sasa ni wakati wa mataifa ya Mashariki ya Kati kutoa shinikizo la juu zaidi la kidiplomasia, kujifunza kutoka kwa Blinken. Chochote kinawezekana katika mwaka wa uchaguzi, na pande zote mbili zitakuwa na hamu ya kuepuka migogoro ya sera za kigeni.

Kucheza mchezo wa kusubiri sio chaguo - watu wa Gaza hawawezi kumudu kusubiri wakati mateso yao yanapoongezeka, na rasilimali zao zinaibiwa na Chevron yenye makao yake California.

Diplomasia ya Blinken imetambulika na kuwa na ubaguzi kwa baadhi ya mataifa ya Kiislamu, huku mataifa mengine ikiwekewa vikwazo. Kutoitikia suala la wakimbizi kutoka Syria, Afghanistan na kwingineko unaonyesha upendeleo wake wa maslahi ya kijiografia na mashirika kuliko yale ya kibinadamu.

Kupatikana maendeleo ya kweli, Blinken na Biden lazima wachukue hatua kwa uwazi, wakitanguliza mahitaji ya Wapalestina na mgawanyo sawa wa rasilimali. Na hio inamaanisha kukomesha kizuizi, kufanya uwekezaji wa muda mrefu, kuunga mkono kujitawala kwa taifa la Wapalestina, na kukomesha ubaguzi unaodhuru jamii asilia na wenyeji.

Kupatikan kwa amani na utulivu, lazima kuwajibishwa Israeli kwa mauaji ya halaiki na ugavi sawa wa nishati , na sio uingiliaji wa kijeshi na unyonyaji wa rasilimali.

Kwa kutanguliza haki, uhuru , na kusitisha unyanyapaa wa makampuni kama Chevron ,ndipo tunaweza kuwa na tumaini wa kumalizika kwa mzunguko wa mateso huko Gaza na kikanda kwa jumla. Ulimwengu unakisia diplomasia kupitia macho ya Marekani, sasa ni wakati wa nchi za Mashariki ya Kati kuchukua hatua madhubuti kabla hazijachelewa.

TRT Afrika