Israeli imewauwa Wapalestina 5 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu

Israeli imewauwa Wapalestina 5 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu

Vita vya Israel dhidi ya Gaza vimeripotiwa kuuwa zaidi ya Wapalestina 47,487.
Wanajeshi wa Israel watumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wapalestina wanaosubiri kuachiliwa kwa mfungwa wa Kipalestina Imad Abu Rumuz nje ya nyumba yake / Picha: AA

Israel imewauwa Wapalestina watano katika mashambulizi huko Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, Wizara ya Afya ya Palestina imesema.

Shambulio la anga la Israeli katika kitongoji cha mashariki cha Jenin lilimuua Ahmad al Sadi mwenye umri wa miaka 16 na kuwajeruhi vibaya watu wengine wawili, wizara hiyo ilisema.

Shambulio la pili ulilenga gari, na kuua watu wawili katika mji wa karibu wa Qabatiya, wizara ilisema, huku la tatu likiwaua watu wawili katikati mwa Jenin.

"Baada ya shambulio liliomuua mtoto (Sadi), shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel lilienga gari huko Qabatiya na kuwaua vijana wawili," gavana wa Jenin Kamal Abu al Rub aliambia shirika la habari la AFP.

"Dakika chache baadaye, shambulio lingine la ndege zisizo na rubani huko Jenin liliwaua vijana wengine wawili waliokuwa kwenye pikipiki."

Hayo yakijiri usitishaji wa mapigano umeingia siku yake ya 15, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema mazungumzo ya awamu ya pili ya usitishaji vita Gaza yataanza Jumatatu.

TRT World