Wanahabari hao waliishutumu BBC kwa kuonyesha msimamo wa kuegemea upande wa Israel/ Picha             

Waandishi wa habari wa BBC walioko nchini Uingereza wamelikosoa Shirika hilo la Utangazaji kwa "upendeleo wake wa kuiunga mkono Israel na kutotoa habari za kutosha kuhusu raia wa Palestina, ikilinganishwa na Waisraeli katika matangazo yao kuhusu suala la Israel na Palestina," Al Jazeera iliripoti.

"BBC ilishindwa kuangazia madai ya Israel kwa kina, haikuweza kutoa taarifa kwa usahihi, na kwa hivyo haikuweza kusaidia umma kuelewa ukiukaji wa haki za binadamu huko Gaza," ilisema barua iliyoandikwa kwa Al Jazeera na wafanyakazi 8 wa BBC siku ya Alhamisi.

Katika barua hiyo, wanahabari hao waliishutumu BBC kwa kuonyesha msimamo wa kuegemea upande wa Israel.

Walidai kwamba wakati BBC ilionyesha mtazamo wa "ujasiri" katika kuripoti juu ya madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa na Urusi nchini Ukraine, lakini ilitumia "sura tofauti" katika kuangazia jinsi raia wanavyochukuliwa katika suala la Israeli-Palestina.

Pia ilihoji ni lini idadi ya Wapalestina waliouawa tangu vita vya Israel dhidi ya Gaza vianze tarehe 7 Oktoba itakuwa kubwa vya kutosha kuleta mabadiliko katika msimamo wa uhariri.

Katika barua hiyo, waandishi wa BBC walisema Shirika hilo linatumia maneno kama "mauaji" na "ukatili" kwa Hamas pekee, wakionyesha kundi la Palestina kama mchochezi pekee na mhusika wa ghasia katika eneo hilo.

Kutoa wito wa ulinzi sawa wa raia

Barua hiyo iliitaka BBC kuakisi vyema matokeo ya ushahidi kutoka kwa mashirika rasmi na yasiyopendelea ya kibinadamu na kuwatendea usawa raia wote katika utangazaji wake wa habari.

Wafanyakazi hao wa BBC ambao hawakutaka kutajwa majina yao pia walitoa wito kwa Shirika la Utangazaji kuhakikisha kuwa utangazaji unaowatendea usawa raia wote unakuwa katikati ya habari zake na walionyesha wasiwasi wao kwamba matangazo ya kibinadamu kwa raia wa Palestina yalikosekana huku yakitoa habari za kina kwa Waisraeli waliopoteza maisha katika mashambulizi.

Barua hiyo pia ilieleza kuwa BBC haikutoa taarifa muhimu kwa watazamaji wake kuhusu historia ya uvamizi wa Israel na mateso ya Wapalestina.

Msemaji wa BBC alijibu madai hayo, akisema, "Katika kipindi chote cha kuripoti mzozo huo, BBC imeangazia wazi hali mbaya za kibinadamu kwa raia huko Gaza na Israeli."

Msemaji huyo pia alituma mifano kutoka kwa matangazo ya BBC yanayohusiana na vita na orodha ya taarifa za kibinadamu kuhusu mateso ya Wapalestina.

TRT Afrika