Vikosi vya Polisi viliwasili kwenye tukio ambapo baadhi ya magari yalikuwa yamechomwa moto.Picha:AA 

Polisi wa Ubelgiji walitumia maji kutawanya watu katika vurugu iliyosababishwa na wafuasi wanaotetea kikundi cha kigaidi cha PKK ambao walikuwa wanatoa kauli za kichochezi katika mitaa yenye wakazi wenye asili ya Kituruki, katika eneo la Heusden-Zolder katika jimbo la Limburg, karibu na mji mkuu wa Brussels na kuwashambulia.

Kikundi hicho kilikuwa njiani siku ya Jumapili asubuhi, wakiwa kwenye magari yao na bendera zenye kuashiria kikundi cha PKK, na kuanza kutoa kauli za kichokozi baada ya kufika mtaa wenye raia wenye asili ya Uturuki.

Wataruki hao walijibu mapigo, hali iliyosababisha kuibuka kwa vurugu hizo.

Kauli za kichokozi toka kwa wafuasi wa PKK

Iliwalazimu polisi kutumia maji kudhibiti moto uliokuwa umewashwa kwenye baadhi ya magari.

Naibu Meya wa Heusden-Zolder Yasin Gul aliiambia Anadolu kuwa wafuasi hao waliwashambulia raia hao huku wakitoa kauli za kichokozi dhidi yao.

"Kwa miaka 60 sasa, tumeishi kama Waturuki wa Ulaya Magharibi, hatujawahi kuwa na tuko kama hili kwenye eneo hili," amesema Gul.

Kwa mujibu wa Gul, robo ya wakazi wa eneo hilo wana asili ya Uturuki.

Kikundi cha kigaidi cha PKK kimeua zaidi ya watu 40,000, wengi wakiwa watoto na akina mama, ndani ya miaka 35.

TRT Afrika