Wafuasi wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakipeperusha bendera za Uturuki kusherehekea Erdogan akiongoza uchaguzi wa marudio wa urais mjini Berlin, Ujerumani Mei 28, 2023. Picha: AA

Nchini Ujerumani, ambayo ni nyumbani kwa watu wengi zaidi walioishi nje ya Uturuki, mamia ya Waturuki waliingia barabarani kusherehekea ushindi wa Rais Recep Tayyip Erdogan katika uchaguzi.

Katika mji mkuu Berlin, wafuasi wa Chama cha AK walisherehekea Jumapili jioni katika vitongoji vyenye watu wengi wa Kituruki, kama vile Kruezberg, kwa kuimba nyimbo na kupeperusha bendera na mabango.

Katika Kurfurstendamm, mojawapo ya njia maarufu zaidi za Berlin, wafuasi wa Erdogan wahakikisha wana sikika katika msafara mkubwa wa magari, wakiimba itikadi na kupiga honi za gari zao.

Sherehe pia zilifanyika katika miji mingine, ikiwa ni pamoja na Cologne na Frankfurt.

Kuchaguliwa tena kwa Erdogan kulithibitishwa na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Uchaguzi la Uturuki (YSK) Jumapili jioni.

Kulingana na matokeo yasiyo rasmi, huku 99.43% ya kura zimehesabiwa, Erdogan alishinda kura ya pili kwa 52.14%, wakati mgombea wa upinzani Kemal Kilicdaroglu alipata 47.86%, mkuu wa YSK Ahmet Yener aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ankara.

Mnamo Mei 14, hakuna mgombea aliyeshinda 50% iliyohitajika katika duru ya kwanza, na hivyo kusababisha duru ya pili ya urais, ingawa Erdogan aliongoza kwa 49.52%.

Zaidi ya raia milioni 64.1 wa Uturuki walijiandikisha kupiga kura, wakiwemo zaidi ya milioni 1.92 ambao awali walipiga kura katika vituo vya kupigia kura vya ng'ambo.

TRT World