Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly wamejadili kwa njia ya simu, mvutano wa hivi karibuni kati ya Israeli na Palestina, kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki, siku ya Jumatatu.
Kundi la upinzani la Hamas lenye makao yake Gaza, lilitekeleza operesheni ya Al - Aqsa dhidi ya Israel mapema Jumamosi, huku likifyatua makombora mengi.
Ilisema kuwa shambulio hilo la ghafla lilikuwa ni kulipiza kisasi kwa uvamizi wa msikiti wa Al-Aqsa katika eneo la mashariki mwa Yerusalemu lililokuwa limechukuliwa kwa nguvu na kuongezeka kwa vurugu dhidi ya wahamiaji.
Wakati huo huo, jeshi la Israeli nalo lilizindua operesheni ya kulipiza kisasi, dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Idadi ya Wapalestina waliouawa na vikosi vya Israel huko Gaza imeongezeka hadi 493, wizara ya afya ya Gaza ilisema Jumatatu huku bado mapigano yakiendelea. Aidha, ilisema idadi ya watu waliojeruhiwa iliongezeka hadi 2,751.
Wizara ya mambo ya ndani ya Gaza imesema kuwa Jeshi la Israel "limeongeza mashambulizi yake" dhidi ya Gaza kwa kutekeleza mamia ya mashambulizi.
Jeshi la Israel limesema kuwa limevamia zaidi ya maeneo 500 katika mashambulizi ya usiku huko Gaza, ambayo walitaja kuwa walengwa wake ni Hamas na kundi la Jihadi ya Kiislamu.
Kwa upande wake, Wizara ya Afya ya Israeli imesema kuwa Waisraeli 700 wameuawa na wengine zaidi ya 2,300 wamejeruhiwa katika mapigano hayo.