"Hatutawasamehe magenge ya uhalifu, wauzaji wa dawa za kulevya. Bila kujali kiwango chao, tutavunja vikundi vya uhalifu vilivyopangwa na kuwaleta mbele ya haki." Alisema waziri wa mambo ya ndani Ali Yerlikaya. / Picha: AA Archive

Uturuki imevunja shirika la kimataifa la uhalifu la Comanchero, na kuwakamata watuhumiwa 37 mjini Isanbul, waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amesema.

Comanchero yenye makao yake Australia na kuongozwa na Hakan Ayik, inaendesha shughuli zake kote duniani na inashiriki katika shughuli za uhalifu, pamoja na biashara ya dawa za kulevya, mauaji, wizi wa silaha, uchomaji moto, na utekaji nyara.

"Hatutawasamehe magenge ya uhalifu, wauzaji wa dawa za kulevya. Bila kujali kiwango chao, tutavunja vikundi vya uhalifu vilivyopangwa na kuwaleta mbele ya haki." Alisema Waziri wa Mambo ya ndani Ali Yerlikaya.

Akitoa maelezo zaidi kuhusu kundi hilo, Waziri Yerlikaya ametaja kwamba Mick Hawi anayedaiwa kuwa kiongozi wa shirika la uhalifu wa kimataifa, Mick Hawi, aliuawa mwaka 2018.

Chini ya uongozi wa Mark Douglas Buddle, shirika hilo la uhalifu liliendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za uhalifu duniani kote.

Buddle alikamatwa ndani ya Jamhuri ya Uturuki ya Kupro ya Kaskazini (TRNC) mnamo 2022 na kupelekwa hadi Australia.

Aidha, Hakan Ayik na Duax Hohepa Ngakuru, wanachama wawili wa kundi hilo, walichukua hatamu ya uongozi na kuendelea na shughuli za uhalifu za kundi hilo.

TRT World