Kulingana na takwimu rasmi duniani, Uturuki imetoa msaada mwingi zaidi mjini Gaza, kuliko nchi yoyote ile duniani.
Asilimia 19 ya misaasa kamili ya misaada iliyoingia Gaza ilitokea Uturuki, licha ya vizuizi vilivyoendelea kuwekwa na Israeli, na kuifanya kuwa ya pili baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu, ambayo ilitoa asilimia 27 ya msaada huo, ulisema Uratibu wa Shughuli za Serikali (COGAT) siku ya Alhamisi.
Uturuki ilifuatiwa na Saudi Arabia ikiwa na asilimia 18, kulingana na takwimu kwenye tovuti ya COGAT, ambayo ina uhusiano na Wizara ya Ulinzi ya Israel.
Kati ya magari ya magonjwa 74 zilizoruhusiwa kungia Gaza, saba zilitolewa na Uturuki.
Uturuki, Misiri na Umoja wa Falme za Kiarabu pia zimeratibu shughuli ya kuokoa wagonjwa 3,204 na majeruhi, pamoja na kusaidia kuwasindikiza 725 wengine nje ya Gaza kwa matibabu.
Ankara imeendelea kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo la Gaza chini ya uratibu wa Cairo, tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel, Oktoba 7.
Zaidi ya hayo, Uturuki inaendelea kuwasaidia wagonjwa na majeruhi wengine walioshindwa kupata huduma za afya katikati ya machafuko hayo ambayo yameua watu 32,000.