Thamani ya sekta ya kilimo ilikuwa Lira ya Uturuki bilioni 200 katika kipindi Januari hadi Machi. / Picha: AA  

Uturuki inashika nafasi ya kwanza barani Ulaya na ni kati ya nchi 10 bora duniani mwaka jana, kwa kuvuna mapato makubwa mwaka jana kutoka sekta ya kilimo, Waziri wa Kilimo na Misitu Ibrahim Yumakli amesema.

Kulingana na takwimu za Shirika la Chakula na Lishe na Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia, mapato yatokanayo na kilimo nchini Uturuki, yalifikia dola bilioni 68.5 kwa mwaka 2023, ambalo ni ongezeko la asilimia 16 kutoka mwaka uliopita.

Taasisi ya Takwimu ya Uturuki (TUIK) iliripoti kuwa sekta za kilimo, misitu na uvuvi, zilichangia asilimia 6.2 ya pato la taifa kwa mwaka 2023, chini kidogo kutoka asilimia 6.5 ya mwaka uliopita.

Katika robo ya kwanza ya 2024, kilimo kilichangia asilimia 2.3 ya pato la taifa, ikiwa imepungua kutoka asilimia 5.2 katika robo ya mwisho ya 2023.

Thamani ya sekta ya kilimo ilikuwa Lira za Kituruki bilioni 206 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi.

Licha ya mdodoro wa asilimia 0.2 katika sekta ya kilimo mwaka jana, uchumi wa Uturuki ulikuwa kwa asilimia 4.5.

Hata hivyo, katika robo ya kwanza ya mwaka 2024, sekta ya kilimo ilishuhudia ongezeko la asilimia 4.6, ukilinganisha na kipindi kama hicho hicho kwa mwaka 2023, ikienda juu kwa asilimia 0.5 kwa mwaka uliotangulia, wakati kwa ujumla, uchumi wa Uturuki ulikuwa kwa asilimia 5.7 kwa mwaka, katika kipindi cha Januari jadi Machi 2023.

Serikali yawaunga mkono wakulima

Serikali ya Uturuki imekuwa mstari wa mbele kwa kutua msaada na kuwaunga mkono wakulima kukuza uzalishaji.

Msaada wa kifedha, ruzuku ya pembejeo ya kilimo na mafunzo kwa wakulima yameifanya sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa.

Matokeo yake, uzalishaji wa kilimo umeendelea kuongezeka. Wakulima wa Kituruki wamepanua shughuli zao, wamewekeza katika pembejeo bora zaidi, na kuimarisha mavuno na ufanisi, yenye kukidhi mahitaji ya chakula na kuchangia ukuaji wa uchumi.

Mazao ya ziada yamefungua fursa za mauzo ya nje, na kuzalisha mapato ya ziada.

Teknolojia pia imechukua nafasi muhimu. Ubunifu kama vile kilimo cha usahihi, ufuatiliaji wa ndege nyuki na mifumo ya hali ya juu ya umwagiliaji imeboresha rasilimali na kupunguza upotevu.

Teknolojia hizi huwezesha maamuzi sahihi, kuboresha tija na uendelevu.

TRT Afrika