Uturuki imelaani sheria mpya iliyopitishwa nchini Uruguay yenye kutambua matukio ya 1915 kama mauaji ya "kimbari."
"Tunaikataa na hatuitambui sheria iliyopitishwa na Bunge la Uruguay na kuidhinishwa na Kaimu Rais wa Uruguay'," imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki katika taarifa yake siku ya Jumanne.
Ikisisitiza kuwa sheria hiyo inakinzana na sheria za kimataifa, hasa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1948, wizara hiyo ilisema illita sheria hiyo kuwa ni "batili."
“Wanasiasa na mabunge hawana mamlaka ya kutoa hukumu kuhusu masuala ya kihistoria yenye utata,” iliongeza.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, hatua hiyo 'haikubaliki' kwani imelenga kuipa Uruguay "faida za kisiasa na kupotosha historia."
Matukio ya 1915
Kuhusu matukio ya 1915, Uturuki inasema vifo vya Waarmenia mashariki mwa Anatolia vilitokea wakati baadhi ya pande ziliunga mkono uvamizi na uasi wa Urusi dhidi ya vikosi vya Ottoman.
Wakati uhamisho wa Waarmenia ulisababisha vifo vingi, Uturuki inapinga uwasilishaji wa matukio hayo kama "mauaji ya halaiki," ikisisitiza kuwa pande zote mbili zilipata hasara katika janga hilo.
Kwa mara kadhaa, Ankara imependekeza kuundwa kwa tume ya pamoja ya wanahistoria kutoka Uturuki na Armenia na wataalamu wengine ili kukabiliana na suala hilo.