Mamlaka ya Uturuki yanatumia neno "kukata makali" kumaanisha kwamba magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au kutekwa. / Picha: AA

Vikosi vya usalama vya Uturuki vimewakata makali jumla ya magaidi 17 wa PKK/YPG kaskazini mwa Iraq na kaskazini mwa Syria, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya nchi hiyo.

Wizara hiyo iliripoti Jumapili kwamba magaidi 15 wa PKK walilengwa katika maeneo ya Gara, Metina, na eneo la operesheni ya "Claw-Lock" kaskazini mwa Iraq. Magaidi wawili waliosalia wa PKK/YPG walilengwa huko Manbij, kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi wa Uturuki wataendelea na mapambano yao bila kuchoka dhidi ya magaidi, popote pale walipo, wizara hiyo ilisema.

Mamlaka ya Uturuki yanatumia neno "kukata makali" kumaanisha kwamba magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au kutekwa.

Operesheni za Uturuki zimekaribia kukomesha uwepo wa PKK ndani ya nchi. Kundi hilo la kigaidi sasa linaendesha shughuli zake kutoka nje ya mpaka. Magaidi mara nyingi hujificha kaskazini mwa Iraq, nje ya mpaka wa Uturuki, kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Uturuki.

Uturuki mnamo 2022 ilizindua Operesheni "Claw-Lock" kulenga maficho ya kikundi cha kigaidi cha PKK katika maeneo ya kaskazini mwa Iraq ya Metina, Zap na Avasin-Basyan.

Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU - imehusika na vifo vya karibu watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, na watoto. Kundi la YPG ni tawi la PKK nchini Syria.

TRT World