Uturuki yakata makali magaidi kadhaa wa PKK/YPG katika muda wa wiki moja

Uturuki yakata makali magaidi kadhaa wa PKK/YPG katika muda wa wiki moja

Jumla ya magaidi waliokatwa makali mwaka huu kaskazini mwa Iraq na Syria imefikia 1,763.
Mamlaka ya Uturuki yanatumia neno "kukamata makali" kumaanisha kwamba magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au kutekwa. / Picha: AA

Vikosi vya usalama vya Uturuki vimewakata makali magaidi 38 wa PKK/YPG kaskazini mwa Iraq na kaskazini mwa Syria katika muda wa wiki moja iliyopita, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya nchi hiyo iliripoti.

"Hivyo, idadi ya magaidi waliokatwa makali kaskazini mwa Iraq na Syria tangu Januari 1 imefikia 1,763, kutoa Iraq ni 868 na kutoka kaskazini mwa Syria ni 895," msemaji wa wizara na Afisa wa Jeshi la Majini Zeki Akturk alisema katika mkutano wa kila wiki wa waandishi wa habari katika mji mkuu Ankara siku ya Alhamisi.

Akturk ameongeza kuwa watu 337 wakiwemo wanachama wanane wa makundi ya kigaidi walikamatwa walipokuwa wakijaribu kuvuka mpaka kinyume cha sheria katika kipindi cha wiki moja iliyopita, huku wengine 1,381 wakizuiwa kuvuka.

“Idadi ya watu waliokamatwa wakijaribu kuvuka mipaka yetu kinyume cha sheria tangu Januari 1, 2024, imeongezeka hadi 8,673, na idadi ya watu waliozuiwa kuvuka mpaka imefikia 70,712,” alisema.

Mkataba na Iraq

Kuhusu mkataba wa makubaliano uliotiwa saini na Iraq kuhusu ushirikiano wa kijeshi, usalama na kukabiliana na ugaidi, Akturk alisema usalama utaimarika kwa mataifa yote mawili.

Uturuki na Iraq zinatazamiwa kuanzisha kituo cha pamoja cha kuratibu usalama mjini Baghdad na kituo cha pamoja cha mafunzo na ushirikiano huko Bashika, ambacho kitarahisisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika mapambano dhidi ya ugaidi, kwa kuzingatia hasa kukabiliana na PKK.

Katika kampeni yake ya takriban miaka 40 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU - imehusika na mauaji ya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto na watoto wachanga. Kundi la YPG ni tawi la PKK nchini Syria.

Wakati huo huo, vyanzo vya usalama vya Uturuki vilisema kuwa Uturuki inafuatilia kwa karibu shughuli za hivi karibuni katika kisiwa cha Cyprus na vitendo vya utawala wa Kigiriki wa Cyprus.

Walisema hatua zinazohitajika zimewekwa ili kuwalinda raia wa Uturuki katika kisiwa hicho, na kuongeza kuwa kwa sasa hakuna wasiwasi wowote wa kiusalama.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT World