Mkataba wa CFE uliandaliwa na kuidhinishwa mjini Istanbul mwaka 1999./ Picha: AA  

Uturuki imejiondoa kwenye mkataba wa Majeshi ya Ulinzi ya Ulaya (CFE).

"Imeamuliwa kusitisha utekelezwaji wa mkataba kati ya Jamhuri ya Uturuki na nchi zingine ambazo ni sehemu ya Mkataba huo toka Aprili 8, 2024 kwa kuzingatia agizo la Rais namba 9,” kulingana na gazeti la Serikali nchini.

Mnamo 1999, mkataba uliohuishwa wa CFE uliandaliwa na kuidhinishwa huko Istanbul, kwa kuzingatia hali halisi mpya kama vile kuvunjika kwa Mkataba wa Warsaw na upanuzi wa NATO.

Urusi pia ilijiondoa kwenye mkataba huo mwaka 2023, huku ikiilaumu Marekani kwa kudharau usalama wa vita baridi na kuongezeka na kupanuka kwa muungano wa kijeshi wa NATO.

Pia, mwezi uliopita Poland ilijiondoa kwenye mkataba huo.

Mkataba wa CFE

Mkataba huo wa 1990 kuhusu Vikosi vya Wanajeshi vya Kawaida barani Ulaya (CFE), uliotiwa saini mwaka mmoja baada ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin, uliweka mipaka inayoweza kuthibitishwa kwenye vipengele vya zana za kawaida za kijeshi ambazo NATO na Mkataba wa wakati huo wa Warsaw zinaweza kupeleka.

Mkataba huo uliandaliwa kuzuia pande zote za Vita Baridi kutokuongeza vikosi zaidi vya kijeshi ili kuwashambulia wengine huko Ulaya.

Uliweka mipaka vya aina tano kuu za kijeshi vya kawaida huko Ulaya-vifaru vya kijeshi, mizinga, magari ya kivita, helikopta na ndege za kivita - na kuamuru uharibifu wa silaha nyingi.

TRT Afrika