Uhusiano wa kiuchumi kati ya Uturuki na Ukraine umekua kwa kasi, hata katikati ya mzozo unaoendelea. Mnamo 2023, biashara ya nchi mbili ilifikia dola bilioni 7.3. / Picha:  AA

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan anatazamiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Andriy Sibiha tarehe 21 Oktoba, ikiwa ni ziara ya kwanza rasmi ya Sibiha nchini Uturuki. Majadiliano yataangazia uungaji mkono wa Uturuki kwa uhuru wa Ukraine, wito wake wa azimio la kidiplomasia kwa vita, na kuimarisha uhusiano wa nchi mbili.

Ziara hii inafuatia safari ya mwezi Agosti ya Fidan nchini Ukraine, nchi hizo mbili zikilenga kuimarisha ushirikiano, hasa katika sekta za uchumi, nishati na ulinzi. Mkataba wa Maelewano na mpango wa mashauriano wa 2025-2026 unatarajiwa kutiwa saini.

Tangu Uturuki na Ukraine ziboreshe ushirikiano hadhi kuwa wa Kimkakati mwaka 2011, maendeleo makubwa yamepatikana katika sekta mbalimbali, ulinzi na nishati zikiwa mstari wa mbele.

Waziri Fidan alikutana na Sibiha mara ya mwisho mnamo Oktoba 2024 wakati wa Mkutano wa Kilele wa Ukraine-Ulaya ya Kusini-Mashariki huko Dubrovnik.

Wakati vita vikiendelea, masuala ya usalama wa kikanda na mipango ya amani imepawa kipao mbale.

Mkutano ujao unatarajiwa kuimarisha zaidi nafasi ya Uturuki kama mpatanishi, kuunga mkono juhudi za azimio la amani kupitia sheria za kimataifa.

Ushirikiano wa Kiuchumi na Mkataba wa Biashara Huria

Uhusiano wa kiuchumi kati ya Uturuki na Ukraine umekua kwa kasi, hata katikati ya mzozo unaoendelea. Mnamo 2023, biashara ya nchi mbili ilifikia dola bilioni 7.3.

Majadiliano katika ziara hiyo huenda yakalenga Mkataba wa Biashara Huria kati ya mataifa hayo mawili, unaotarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.

Makubaliano hayo yanaonekana kuwa hatua muhimu katika kukuza biashara ya nchi mbili na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi katika muda mrefu.

Uturuki imekuwa na nafasi muhimu katika kuwezesha juhudi za kidiplomasia na kibinadamu wakati wa vita. Mnamo 2022, iliandaa mikutano ya kwanza kati ya wawakilishi wa Kiukreni na Urusi.

Zaidi ya hayo, juhudi za Uturuki katika Ukanda wa Nafaka wa Bahari Nyeusi, ambazo ziliwezesha usafirishaji wa tani milioni 33 za nafaka za Kiukreni, zimekuwa muhimu katika kupunguza uhaba wa chakula duniani.

Uturuki pia imehusika katika kuandaa mazungumzo ya wafungwa kati ya Ukraine na Urusi, na kuangazia zaidi msimamo wake wa dhati katika juhudi za amani za kikanda.

Ziara hii inatarajiwa kuimarisha dhamira ya Uturuki katika uhusiano wa nchi mbili na utulivu mpana wa kikanda, kuendelea na jukumu lake kama mhusika mkuu katika kupatanisha amani na kuunga mkono Ukraine.

TRT World