Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesema Uturuki itaungana na Afrika Kusini katika kesi ya mauaji ya halaiki dhidi ya Israeli katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa.
"Uturuki itaungana na Afrika Kusini katika kesi ya mauaji dhidi ya Israel katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa," amesema Fidan Jumatano.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari baada ya mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Retno Marsudi wizarani, Fidan alielezea kuhusu jambo hilo, akigusia majadiliano yaliyofanyika katika ziara yake ya hivi karibuni ya Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia.
Fidan amesema katika kufanya majadiliano ya kidiplomasia na nchi zinazotambua Palestina kama taifa, ikiwemo Jumuia ya nchi za Kiislamu, baadhi ya nchi imeonyesha utayari wa kuchukua hatua kuhusiana na jambo hilo.