Israel imekanusha kuhusika na shambulio hilo la anga, huku wahusika wengi wa kimataifa wakitaka uchunguzi usio na upendeleo kuthibitisha ni nani anayehusika. / Picha: AA

Uturuki inatarajiwa kutangaza kipindi cha maombolezi ya kitaifa ya siku tatu kuonyesha mshikamano na Palestina kufuatia shambulio la anga la Israel dhidi ya hospitali ya Al Ahli Arab huko Gaza ambalo liliua watu wasiopungua 500.

Amri ya rais inatarajiwa kutangazwa kujibu mashambulio yasiyokoma ya Israeli huko Gaza, alisema mbunge wa Uturuki na naibu mwenyekiti wa kikundi cha chama cha AK Ozlem Zengin, Jumatano.

Aliongeza kuwa bunge zima limelaani mauaji kwa pamoja kwenye taarifa yao kuhusu mashambulizi ya Israeli dhidi ya hospitali, na kusisitiza kuwa mabomu kwenye vifaa vya matibabu ni kinyume cha sheria za vita.

Uturuki, imelaani vikali shambulio hilo huku rais Recep Tayyip Erdogan akitoa wito kwa wanadamu wote kuchukua hatua za kukomesha "ukatili wa Israel usio na kifani nchini Gaza".

"Kuvamia hospitali yenye wanawake, watoto, na raia wasio na hatia ni mfano wa hivi karibuni wa mashambulizi ya Israeli bila maadili ya msingi ya kibinadamu," Erdogan alisema kwenye mtandao wa X kufuatia shambulio hilo.

"Kulipua hospitali kwa mabomu ni uhalifu mkubwa. Kuuwa watu ambao wanapokea matibabu ni uchungu mkubwa. Kulenga raia ni kutumia mbinu za ugaidi, kwa wazi na rahisi, " Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun pia alisema katika taarifa kupitia X.

Madai ya Israeli yakosolewa

Israel imekanusha kuhusika na shambulio hilo la anga, huku washikadau wengi wa kimataifa wakitaka uchunguzi usioegemea upande wowote wa kuthibitisha ni nani anayehusika ufanyike.

Wakati huo huo, kitengo cha serikali ya Uturuki cha kupambana na habari potofu kimekataa madai "ya uwongo" ya Israeli ya kwamba Hamas ilitekeleza shambulio la anga.

"Madai ya kwamba' (Kundi la Palestina) Hamas, sio Israeli, ndilo lilifanya shambulio hilo 'kwenye hospitali ya Al Ahli Arab ilichoko kitongoji cha Al Zaytoun, Gaza ni ya uwongo," Kitengo cha kurugenzi ya mawasiliano ya kupambana na habari potofu kilisema Jumanne kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii, X.

"Eneo la Al zaytoun kaskazini mwa Gaza ni eneo ambalo mamia ya raia wameuawa katika siku za mashambulizi makali ya Israel," iliongeza.

"Wakati picha za bomu la hospitali zinapochunguzwa, inakuwa dhahiri kwamba risasi ambazo zilikuwa na athari ya kuharibu eneo hilo sio aina ambayo Hamas ilikuwa imetumia hapo awali," taarifa hiyo ilisisitiza.

Uchambuzi wa machapisho ya uwongo ya vyombo vya habari uligundua kuwa "picha zilizoenezwa na akaunti za propaganda za Israeli zinazodai kuwa 'Kombora la Hamas liligonga hospitali' zilikuwa kutoka 2022, sio 2023," kitengo cha kupambana na habari potofu kiliongeza.

Shambulio hilo la anga lilikuja siku ya 12 ya mzozo kati ya Israel na Hamas, huku wito wa kimataifa inayoongezeka ya makundi yasiyo ya kiserikali na viongozi wa dunia, wakisema kampeni ya mabomu ya Israel kwenye eneo lililozingirwa – ikiwa ni pamoja na vituo vya afya, makazi, na nyumba za ibada-inakiuka sheria za kimataifa na inaweza kuwa uhalifu wa vita.

AA