Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa serikali ya Uturuki itaendelea kusimama na Libya kufuatia janga la mafuriko ya nchi hiyo, huku akiongeza kuwa ameamuru uhamasishaji wa rasilimali zote za serikali kuwasaidia Walibya.
Akizungumza kwenye mkutano wa mabadiliko ya mijini na tetemeko la Ardhi jijini Istanbul, Rais Erdogan amesema; "Kufikia Sasa, Uturuki imetuma ndege tatu na meli tatu kama sehemu ya misaada ya kibinadamu kwa taifa la Libya lililoathiriwa na mafuriko."
"Msaada wetu kwa ndugu na dada zetu wa Libya utaendelea bila mapumziko ili kuwasaidia wapate nafuu katika siku hizi ngumu haraka iwezekanavyo," aliongeza.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi, takriban watu 6,000 wameuawa na maelfu hawajulikani waliko mpaka sasa kutokana na mafuriko yaliyoshuhudiwa mwishoni mwa wiki iliyopita mashariki mwa Libya.
Mvua kubwa na mafuriko yaliyotokana na Dhoruba Daniel yalikumba maeneo kadhaa siku ya Jumapili mashariki mwa Libya, hasa Benghazi, Al-Bayda, Al-Marj, pamoja na Soussa na Derna.
Sheria za Kufanya Uturuki kustahimili tetemeko la ardhi
Erdogan ameongeza kuwa Uturuki itaongeza juhudi zake ili kuifanya nchi hiyo kustahimili tetemeko la ardhi.
"Lengo la sheria ya tetemeko la ardhi ni "kuanzisha kujenga miundombinu kisheria ambayo itafanya mabadiliko ya mijini kwa njia salama zaidi, kwa kasi zaidi, na ya haki dhidi ya ukweli wa kumudu tetemeko ya ardhi", alisema.
"Kuanzia sasa, tunahitaji kufanya kazi hiyo kwa kutambua kuwa majimbo yetu yote 81 ya nchi yetu kuwa maeneo yenye hatari ya kukumbwa na janga la tetemeko la ardhi," Erdogan aliongeza.
Kufuatia Februari 6, matetemeko ya ardhi kusini mwa Uturuki, Erdogan alisema kuwa nchi hiyo inajenga upya yaliyoathiriwa na tetemeko kubwa kama nchi ya ukubwa wa kati.
Uturuki ni mojawapo ya maeneo yenye matetemeko mengi zaidi ulimwenguni. Mnamo Februari, matetemeko makubwa ya ardhi kusini mashariki mwa Uturuki yaliwaua zaidi ya watu 50,000.
Mnamo 1999, tetemeko kubwa lilitokea Kaskazini-magharibi mwa Uturuki, na kuua zaidi ya watu 18,000.