Ulinzi, uhamaji vyatawala mkutano wa viongozi wa Ujerumani na Uturuki

Ulinzi, uhamaji vyatawala mkutano wa viongozi wa Ujerumani na Uturuki

Kansela wa Ujerumani atakuwa na mazungumzo na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan jijini Istanbul.
Rais wa Uturuki Erdogan akiwa na Kansela wa Ujerumani Scholz wakati wa ziara yake jijini Ankara./Picha:  Reuters  

Suala la Ulinzi na Uhamaji vitatawala ajenda ya mazungumzo kati ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan jijini Istanbul, siku ya Jumamosi.

Ziara hiyo inakuja wakati kukiwa na ongezeko la uhasama katika eneo la Mashariki ya Kati.

“Tutaangazia masuala mbalimbali. Suala la uhamaji ni mojawapo ya masuala yatakayojadiliwa,” alisema Scholz kabla ya ziara hiyo, ambayo ni ya pili nchini Uturuki toka Machi mwaka 2022.

Suala la Ujerumani kuiuzia ndege za kivita Uturuki, pia litatawala mazungumzo hayo, alisema.

“Kimsingi, tutajadiliana suala la kuwapa sialha kwa washirika wenzetu wa NATO,” alisema, akiongeza kuwa Uingereza inafanya mazungumzo na serikali ya Uturuki kuhusu kuuziana ndege za kivita.

“Hiyo ni hatua ya wazi, na ndicho alichokisema, ‘wacha tukubaliane,’” alisema.

Ndege za kivita aina ya Typhoon zinatengenezwa kwa pamoja nchini Uingereza, Ujerumani, Italia na Hispania.

Mauaji ya halaiki ya Israeli dhidi ya Gaza yameathiri uhusiano kati ya Uturuki na Ujerumani, ambayo ni msambazaji mkubwa wa silaha kwa Tel Aviv.

Kwa muda mrefu, Erdogan amekuwa ni mkosoaji mkubwa wa vita vya kinyama vya Israeli na uvamizi wake wa hivi karibuni nchini Lebanon, huku akimlinganisha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kiongozi wa Nazi Adolf Hitler.

Licha ya ziara ya Kansela huyo kukamilishwa kabla ya Israeli haijamuua kiongozi wa kisiasa wa Hamas Yahya Sinwar, mapigano yanayoongezeka ya Tel Aviv katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na Lebanon huenda yakaibuka wakati wa majadiliano.

Suala la uhamaji

Kulingana na Scholz, ziara yake ya Istanbul itakuwa ni fursa ya kujadiliana suala la ushirikiano kati ya Uturuki na Umoja Ulaya, hususani suala la uhamaji.

“Mara zote, nimeheshimu suala hili na kuiomba jumuiya ya Ulaya kuongeza mkakati huu,” alisema akizungumzia mkataba wa 2016 kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya ambao ulizuia wakimbizi kuingia Ulaya kupitia bahari ya Aegean.

Hata hivyo, Ankara imekuwa ikituhumu washirika wenzake wa Ulaya kwa kushindwa kuheshimu mkataba huo.​​

Kama sehemu ya makubaliano hayo, Umoja wa Ulaya umekuwa ukiahidi kuharakisha mchakato wa kujiunga na Umoja wa Ulaya wa Uturuki, kuanza mazungumzo juu ya kufanya makubaliano ya biashara ya Umoja wa Forodha kuwa ya kisasa na kutoa usafiri usio na visa kwa raia wa Uturuki ndani ya eneo la Schengen.

Takribani watu milioni 3 nchini Ujerumani, wana asili ya Uturuki.

TRT Afrika