Rais Erdogan amesisitiza kuwa ugaidi si suala la kisiasa linalopaswa kuchukuliwa kitofauti./ Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonesha nia ya kuondoa vitisho vya kigaidi sio nchini Uturuki pekee, bali katika kanda nzima.

"Tumeazimia kuonesha kuwa ugaidi hauna nafasi katika mustakabali wa Uturuki na ukanda mzima. Azma hiyo imeimarishwa kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni," alisema Erdogan wakati wa risala yake aliyoitoa katika futari ya pamoja na maofisa wa usalama katika mji mkuu wa Ankara siku ya Jumatano.

Pia amesisitiza kuwa ugaidi si suala la kisiasa linalopaswa kuchukuliwa kwa utofauti.

Erdogan amesema vikundi vyote vya kigaidi vikiwemo PKK, FETO, Daesh, na DHKP-C, ni adui kwa watu wa Uturuki.

Katika operesheni yake ya kigaidi ya miaka 40 dhidi ya Uturuki, kikundi cha PKK kimeorodheshwa kama cha kigaidi katika nchi za Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, ikuhusishwa na vifo vya zaidi ya watu 40,000, wengi wakiwa ni wanawake, watoto na wachanga.

FETO na kiongozi wao anayeishi Marekani Fetullah Gulen walisuka mipango ya jaribio la mapinduzi lililoshindikana la Julai 15, 2026 nchini Uturuki, ambapo watu 252 walipoteza maisha huku wengine 2,734 wakijeruhiwa.

TRT Afrika