Tukio la kigaidi la Ankara limezidi kuimarisha utayari wa Uturuki wa kumaliza ugaidi, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.
“Tukio hili la kidhalimu limezidi kutupa nguvu ya kuondoa ugaidi,” amesema Rais Erdogan siku ya Alhamisi wakati wa mkutano wa BRICS nchini Urusi.
Erdogan aliwashukuru "marafiki" wote kwa salamu zao za rambirambi na mshikamano waliouonesha baada shambulizi la kigaidi siku ya Jumatano jijini Ankara.
Watu wapatao watano na wengine 22 walijeruhiwa katika shambulizi la kigaidi kwenye makao makuu ya shirika la Aerospace Industries (TAI) katika mji mkuu Ankara.
Israeli yahatarisha vita zaidi
Akizungumzia mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza na Lebanon, Erdogan alisema: "Maadamu umwagaji damu katika Mashariki ya Kati hautakomeshwa, hakutakuwa na mazungumzo ya haki, amani, au maendeleo kwa siku zijazo."
“Uchokozi wa Israeli umewasha moto katika kanda nzima, umevuka mipaka, hususani sheria na dhamira,” alisema Erdogan.
"Watu wa Palestina wanakabiliwa na mauaji ya halaiki huko Gaza. Kwa kuishambulia Lebanon, Israeli imezidisha ukatili huo,” alibainisha Erdogan.
"Uanzishwaji wa Palestina huru na inayojitegema, ikis linalojitegemea, huru na linaloshikamana kijiografia na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake kwa misingi ya mipaka ya 1967 ni muhimu kwa amani ya kudumu na ya haki katika eneo hilo," alisisitiza.
Erdogan alizitaka nchi zote ambazo hazijaitambua Palestina kama taifa huru kufanya hivyo.
“Kuendelea kuioa Israeli silaha bila masharti yoyote kunaendelea kuwafanya kutekeleza mashambulizi kiholela,” alisema.
Nafasi ya BRICS
"Tumezindua mpango katika Umoja wa Mataifa wa kusitisha uuzaji wa silaha kwa Israel," Erdogan alisema, na kuongeza: "Nina imani nchi wanachama wa BRICS watatoa msaada katika suala hili."
"Utaratibu wa kimataifa wa haki na maendeleo unaweza kupatikana tu kwa kuwa na amani na usalama nje ya mipaka yetu," alisema Erdogan.
Jeshi la Israeli limeendeleza mashambulizi ya kikatili huko Gaza tangu shambulio la kuvuka mpaka la kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas Oktoba mwaka jana, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano.
Watu wapatao 42,800 wameuwawa tangu kuanza kwa mashambulizi hayo, wengi wakiwa ni wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 100,400 wakijeruhiwa, kulingana na mamlaka za afya.
"Tunaamini kwamba BRICS imetoa michango isiyo na kifani katika kujenga utaratibu wa haki wa kimataifa kwa kuhudumia maendeleo ya biashara ya kimataifa, ukuaji wa uchumi, na malengo ya maendeleo endelevu," Erdogan alisema.
"Kama Uturuki, tumedhamiria kuendeleza mazungumzo yetu na familia ya BRICS, ambayo tumeanzisha uhusiano wa karibu kulingana na kuheshimiana na kanuni za kushinda," rais aliongeza.