Mama Emine Erdogan / Picha: AA

Mke wa rais wa Uturuki, Emine Erdogan amewakumbuka watoto wa Kipalestina waliouawa huko Gaza kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israeli kwenye eneo lililozingirwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya watoto duniani, Novemba 20

"0, 1, 3, 5, 6, 8, 9 ... hizi sio nambari tu. Wanawakilisha idadi ya maelfu ya watoto huko Gaza, ambayo imekuwa ikishambuliwa na Israeli tangu Oktoba 7," aliandika.

Haki yao ya msingi, haki ya kuishi, imenyakuliwa," Erdogan alisema Jumatatu kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa X.

"Tumechelewa sana kuwasaidia watoto wanaowafariji ndugu zao kwa maneno, 'msiwe na wasiwasi; tutakufa hivi karibuni," aliongeza.

"Hii ni aibu kubwa na ya kutisha kwa ubinadamu kwa ujumla."

Mama huyo wa taifa alisema Novemba 20 mwaka huu ni siku ya "Giza" kwa watoto duniani, wakati watoto wa Palestina hawana uhakika wa kuiona kesho kwa kunusurika mashambulizi ya Israeli.

"Kadiri muda unavyokwenda kwa watoto wasio na ulinzi wanaoishi Gaza, wacha sote tupige kelele' kusitisha mapigano sasa' kwa sauti kubwa zaidi, haswa leo!"

Mama Emine Erdogan alitaka kushuhudia ulimwengu unaofaa kuishi kwa kila mtoto.

Maelfu ya majengo muhimu, ikiwemo pamoja na hospitali, misikiti na makanisa, pia kuharibiwa katika mashambulizi ya anga na ardhi ya Israeli dhidi ya eneo lililozingirwa.

Vikwazo vya Israeli pia vimezuia Gaza kutokuwa na mafuta, umeme na maji, na kupunguza utoaji wa misaada kwa mtiririko mdogo.

TRT World