Katika mkutano huo, Erdogan alisisitiza umuhimu wa ujumbe wa nchi za Kiislamu kuwaunga mkono Wapalestina / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na mwenzake wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud katika mkutano wa faragha katika Ikulu ya Istanbul Dolmabahce.

Mkutano wa Ijumaa ulijumuisha Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa wa Uturuki Yasar Guler na Waziri wa Viwanda na Teknolojia Mehmet Fatih Kacır, ilisema Ikulu ya Uturuki.

Marais hao walijadili mashambulizi ya Israel katika maeneo ya Wapalestina, juhudi za Uturuki kupeleka misaada ya kibinadamu katika Gaza ya Palestina, na hatua zinazohitajika kwa ajili ya kusitisha mapigano ya kibinadamu, kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Katika mkutano huo, Erdogan alisisitiza umuhimu wa ujumbe wa nchi za Kiislamu kuwaunga mkono Wapalestina.

Amani ya kudumu na utulivu katika kanda inaweza tu kukamilika kwa umoja, Erdogan alisema.

Uhusiano ya Uturuki na Somalia

Mkutano huo pia ulizungumzia hatua zinazoweza kuchukuliwa katika uhusiano wa Uturuki na Somalia, kukabiliana na ugaidi, na ushirikiano wa kiuchumi.

Uturuki, mshirika wa karibu wa Somalia, amewekeza katika elimu, miundombinu na huduma za afya za taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Msaada wa kibinadamu wa Kituruki na maendeleo ya kiufundi kwa Somalia katika muongo uliopita umezidi dola bilioni moja , Erdogan alisema mwaka jana.

Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, kiasi cha biashara cha nchi hizo mbili mwaka 2022 kilikuwa dola milioni 363, kutoka dola milioni mbili mwaka 2003, na kuna dola milioni 100 za uwekezaji wa Uturuki nchini Somalia.

Uturuki ina Ubalozi wake mkubwa zaidi barani Afrika huko Mogadishu na pia ilijenga kituo chake kikubwa zaidi cha kijeshi cha nje ya nchi huko ili kutoa mafunzo kwa jeshi la taifa la Somalia.

TRT Afrika