Julai iliyopita, Uturuki Na Misri ziliibua uhusiano wao wa kidiplomasia na kuteua mabalozi. / Picha: AA

Rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema majaribio ya kuwahamisha watu wa Gaza, Palestina kutoka nchi yao ni " ya bure na yasiyo na maana.”

Erdogan amesema kuondolewa kwa idadi ya watu kwa nguvu huko Gaza "hakukubaliki," katika mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Misri Abdel Fattah el Sisi huko Cairo, siku ya Jumatano.

"Tunatoa kipaumbele juhudi za kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa Gaza bila vikwazo vyovyote," alisema.

Pia aliongeza kuwa Uturuki itaendelea kushirikiana na kusimama kwa mshikamano na "ndugu zake wa Misri" ili kukomesha umwagaji damu huko Gaza.

Mnamo mwezi Julai mwaka uliopita, Uturuki na Misri zilifufua uhusiano wao wa kidiplomasia na kuteua mabalozi.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulikuwa katika kiwango cha manaibu wa mabalozi tangu 2013.

TRT World