Rais Erdogan azungumza na kiongozi wa UAE  - AL Nahyan. Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo kupitia njia ya simu na Kiongozi wa Falme za Kiarabu (UAE), Mohammed bin Zayed Al Nahyan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ya Uturuki, maendeleo ya hivi karibuni katika mchakato wa kusuluhisha migogoro kati ya Israeli na Palestina yalijadiliwa kwenye mkutano huo.

Wakizungumza kwa njia ya simu, wawili hao walijadili matukio ya hivi karibuni katika mchakato wa mzozo kati ya Israeli na Palestina, huku Rais Erdogan akisema kuwa usitshwaji wa mvutano unawezekana iwapo hatua bora za kimataifa zitachukuliwa

AA