Rais Erdogan alisema kuwa licha ya kwamba Alper Gezeravci alipata changamoto, itakuwa ni faida kwa Atasever akifuata nyayo za mtangulizi wake/ Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemtakia heri mwanaanga wa pili wa nchi hiyo Tuva Cihangir Atasever na kusema: "Wewe ni mwanaanga wetu wa pili lakini hutokuwa wa mwisho."

Rais Erdogan alikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Atasever siku ya Ijumaa, kabla ya safari yake ya anga za mbali siku ya Jumamosi, kutoka kituo cha Spaceport kilichopo New Mexico, nchini Marekani, ili kumjulia hali na kufahamu maandalizi ya misheni hiyo.

Kwa upande wake, Atasever alimjullisha Rais kwamba wako tayari kwa safari hiyo, huku akijinisabu kwa mafunzo makali ya utayari, aliyoyafanya pamoja na Alper Gezeravci, mwanaanga wa kwanza wa Uturuki.

"Pamoja na wewe, nchi yetu sasa itatayarisha msingi kwa ajili ya misheni ya tatu ya anga za juu. Ninaamini hili; wewe ni kijana mwenye nguvu, na unaye Alper kama kiongozi wako. Nakutakia safari ya mafanikio," alisema Erdogan.

Rais alibainisha kuwa wakati wa misheni hiyo, Atasever atabeba bendera ya Azerbaijan na ile ya Uturuki kwani mama yake ni pamoja na bendera ya Uturuki kwenye misheni yake, kutokana na mama yake kuwa Mwazerbaijan.

"Utawakalisha ndugu wote wawili," Erdogan aliongeza, akisisitiza umuhimu wa misheni hiyo kuendeshwa kwa kuzingatia kauli mbiu ya "dola mbili , taifa moja," na kumtakia Atasever kila la heri.

TRT Afrika