Ndege ya Shirika la Ndege la Israeli EI, imelazimika kutua kwa dharura katika mji wa kusini magharibi ya Uturuki, Antalya ili kutoa huduma ya kitabibu kwa abiria wake, kisha kuondoka bila kujaza mafuta, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki.
Ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari yake kati ya Warsaw kuelekea Tel Aviv ilitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Antalya baada ya abiria wake kuugua.
Vyanzo vya kidiplomasia vimethibitisha kuwa ndege hiyo iliruhusiwa kutua ili kutoa msaada kwa abiria huyo.
"Ruhusa ya kutua kwa dharura ilitolewa kufuatia taarifa za uwepo za abiria aliyeugua ndani ya ndege hiyo. Kwa hali ya kawaida na ya kibinadamu, ndege hiyo ilipaswa kuwekwa mafuta lakini rubani aliamua kuirusha ndege hiyo kabla ya mchakato huo kukamilika," kilisema chanzo hicho.