Watu 27 wamepoteza maisha na wengine 3 kujeruhiwa kufuatia jengo moja katika wilaya ya Besiktas kushika moto, ofisi ya Gavana wa Istanbul imesema.
Idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 27, huku waliojeruhiwa wakiwa ni 3, ilisema ofisi ya Gavana Davut Gul siku ya Jumanne, na kuongeza kuwa moto huo ulizuka katika sehemu ya chini ya jengo hilo lenye ghorofa 16.
Majeruhi waliwahishwa kwenye hospitali za jirani kwa ajili ya matibabu, ilisema ofisi hiyo.
Moto huo ulidhibitiwa na vikosi vya Zimamoto ambavyo vilivyohusisha zimamoto 86 na magari 31.
Moto huo ulizuka wakati wa matengenezo katika eneo la burudani lililoko kwenye eneo la chini (-1 na -2) ya jengo hilo, ilisema ofisi ya Gavana huyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun alituma salamu zake za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha katika moto huo huku akiwatakia nafuu ya haraka majeruhi wa tukio hilo, kupitia ukurasa wake wa X.
Altun alisema Rais Erdogan alikuwa anafuatilia kwa ukaribu tukio hilo, huku akiendelea kupokea taarifa kutoka kwa mawaziri na ofisi ya Gavana wa Istanbul.
Uchunguzi wa kina kuhusu tukio umekishaanza, ambapo vipengele vyote vya moto vitachunguzwa, aliongeza.