Mkutano wa nne wa Biashara na Uchumi wa Uturuki-Afrika unatarajiwa kufanyika Istanbul kuanzia Oktoba 12 hadi 13 utaangazia nishati, miundombinu, kilimo, huduma za afya na utalii.
Mkutano huo utahudhuriwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, na mkuu wa Umoja Wa Afrika Azali Assoumani, Waziri wa Biashara wa Uturuki Omer Bolat, na Kamishna Wa Maendeleo ya Kiuchumi, Biashara, Viwanda, na Madini Katika Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Albert Muchanga.
Kongamano hilo la siku mbili, litaandaliwa na bodi ya uhusiano wa nje ya Uturuki maarufu (DEIK) kwa kushirikiana Na Wizara ya Biashara na Jumuiya ya Afrika, huku ikitarajia kuwapokea washiriki 3,000.
Wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali
Mkutano huo wenye kauli mbiu, Kusuluhusha Changamoto, Kufungua Fursa: Kujenga Ushirikiano wa Kiuchumi wa Uturuki-Afrika wenye Nguvu, utatanguliza sekta za nishati, miundombinu, kilimo, biashara ya kilimo, huduma za afya, utalii, na uuzaji wa kidijiti.
Katika siku ya pili ya mkutano huo, wafanyabiashara wa kituruki na Waafrika watapokezana uzoefu wao katika uundaji upya wa mazingira ya ulimwengu wa biashara wakati wa Mazungumzo ya Uongozi wa Wanawake wa Uturuki na Afrika.
Katibu mkuu wa Eneo la Biashara huru la Bara la Afrika (AfCFTA), Wamkele Mene, pia atahudhuria huku akigusia athari za mkataba wa biashara wa Pan-Afrika juu ya biashara kati ya Uturuki na Afrika.