Mfumo wa kimataifa watetea vinara wa vita vya pili vya dunia, Balozi wa Palestina nchini Uturuki asema

Mfumo wa kimataifa watetea vinara wa vita vya pili vya dunia, Balozi wa Palestina nchini Uturuki asema

"Wapalestina wana haki ya kujitawala, eneo hilo litakuwa na utulivu iwapo tu haki hii itakapopatikana," anasema Dk Faed Mustafa.
 "Licha ya mateso na majeraha, tunaendelea katika harakati zetu za kutafuta uhuru katika nchi yetu," balozi wa Palestina anasema.  

Mfumo wa dunia unapendelea mataifa yaliofanikiwa katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Balozi wa Palestina nchini Uturuki, Dkt Faed Mustafa amesema.

Mustafa ametoa kauli hiyo wakati wa hafla maalumu ya Ramadhan iliyoandaliwa kama ishara ya mshikamano kwa watu wa Palestina, na kuandaliwa na Shirika la Habari la Uturuki (TRT), siku ya Ijumaa, mjini Istanbul.

"Msimamo wa Rais Erdogan wa Uturuki, 'dunia ni kubwa kuliko tano ', inajumuisha suala la msingi ya namna mfumo wa kimataifa unavyowalinda washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia pekee," alisisitiza Mustafa.

Matamshi ya balozi wa Palestina yanakuja wakati karibu Wapalestina 32,000 wameuawa katika vita vya Israel dhidi ya Gaza, huku wanawake na watoto wakiwa asilimia 70 ya majeruhi, kama ilivyoripotiwa na Umoja wa Mataifa.

Kuendeleza mchakato wa uhuru

"Dhuluma za Israeli huko Palestina lazima zikome," Mustafa alisisitiza. "Wapalestina wana haki ya kujitawala, na hadi haki hii itakapopatikana, eneo hilo litasalia kutokuwa na utulivu."

Israel ilianzisha mashambulizi yake katika eneo lenye wakazi wengi kufuatia shambulio la kushtukiza katika eneo lake na kundi la Palestina Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, na kusababisha takriban vifo 1,200 kulingana na ripoti za Israeli.

Umoja wa Mataifa umeonya mara kwa mara dhidi ya vitendo vya kiholela au visivyo na uwiano vinavyolenga Gaza, na mapema Januari mwaka huu, Mahakama ya Kimataifa ya Haki ilionesha uwezekano wa Israel kufikia hatua ya kutekeleza mauaji ya kimbari.

"Pamoja na mateso na majeraha yetu, bado tunaendelea na nia ya kutafuta uhuru wa ardhi yetu," alisema Balozi huyo wa Palestina.

"Tunajitoa sadaka na hatutoyumba mpaka uhuru upatikane."

Mustafa alimshukuru Rais Erdogan kwa msaada wa hali na mali wa kibinadamu, ikiwemo kutuma ndege na meli Gaza na kupeleka msaada wa matibabu kwa majeruhi wa Kipalestina wanaoendelea kupokea matibabu katika hospitali za Uturuki, toka kuanza kwa mashambulizi hayo.

TRT Afrika